15-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Kitendo chema kinafaa kikiwa kimemshirikisha Allaah?
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu
Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.
Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com
15-Je, Kitendo chema kinafaa kikiwa kimemshirikisha Allaah?
Hapana! Kitendo chema ambacho kina kumshirikisha Allaah hakifai kitu mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).
وَلَوْ أَشْرَكُوا لَحَبِطَ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٨٨﴾
Na kama wangemshirikisha bila shaka yangeporomoka yale waliyokuwa wakitenda. [Al-An’aam: 88]
((من عمِلَ عملاً أشرك معيَ فِيهِ غيري تركتُه وشِرْكَه)) حديث قدسي رواه مسلم.
((Atakayefanya kitendo na huku kanishirikisha Mimi na mwengine, namwacha yeye na mshirika wake)) [Hadiyth Qudsiy ameipokea Muslim]