16-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Shirki ipo kwa Waislamu?
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu
Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.
Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com
16-Je, Shirki ipo kwa Waislamu?
Naam! Shirki ipo kwa Waislamuna masikitiko kuwa ipo tena wanamshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa wingi!
وَمَا يُؤْمِنُ أَكْثَرُهُم بِاللَّـهِ إِلَّا وَهُم مُّشْرِكُونَ ﴿١٠٦﴾
106. Na wengi kati yao hawamwamini Allaah isipokuwa wao ni wenye kufanya shirki. [Yuwsuf: 106]
((لاَ تقوم السّاعة حتّى تلحق قبائل مِن أُمّتي بالمشركين وحتى تُعبَد الأوثان)) صحيح رواه الترمذي.
((Qiyaamah hakitosimama mpaka kutafika wakati watu wa baadhi ya makabila katika ummah wangu wataungana na washirikina na hadi watakapoabudu asiye Allaah! [Swahiyh ameipokea At-Tirmidhiy]