31-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Waumini watamuona Rabb wao watakapoingia Jannah?
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu
Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.
Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com
31-Je, Waumini watamuona Rabb wao watakapoingia Jannah?
Naam. Waumini watamuona Rabb wao watakapoingia Jannah.
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاضِرَةٌ ﴿٢٢﴾
Nyuso siku hiyo zitanawiri.
إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٌ﴿٢٣﴾
Zikimtazama Rabb wake. [Al-Qiyaamah: 22-23]
(إنَّكُمْ سَتَرون رَبكُم) رواه البخاري ومسلم
((Hakika nyinyi mtamuona Rabb wemu)) [Al-Bukhaariy na Muslim]