32-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Waislamu wanapaswa wawe wanahukumu mambo yao kwa kufuata nini?
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu
Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.
Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com
32-Waislamu wanapaswa wawe wanahukumu mambo yao kwa kufuata nini?
Waislamu wanapaswa wahukumu kufuata Qur-aan na Sunnah ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).
وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ
Na wahukumu baina yao kwa yale Aliyoyateremsha Allaah [Al-Maaidah: 49]
((الله هُوَ الْحكم وَإلَيْهِ المَصِير)) حسن رواه أبو داود
((Allaah ndiye mwenye kuhukumu na Kwake ndio marejeo)) [Hadiyth Hasan ameipokea Abuu Daawuwd]