Amezuiliwa Kuonana Na Mama Yake Afanyeje?

 

 

SWALI:

SWALI LANGU NI SOMA KWA MAKINI HALAFU NAOMBA MINIJIBU.

Mimi wazazi wangu upandewa baba hawataki niende wa mama(upande wa mama) ati kwa sababu mama alipoachwa na baba mimi nilikuwa ni mdogo sana mtoto wa mienzi 8  halafu mama akaolwa na mume mwengine halafu akawa hapiti kuja kunitembela. sasamimi nilikuwa najiuliza mimi mama ninae au amekufa.kuna siku moja nilikutana na mjomba kaka ake mama mimi nilikuwa simjui lakini yeye ananijuwa mimi aliniambia kuwa tupange siku tuende kumuona mama kwa vile mimi nilikuwa simjui mama nikamuambia hamna shida mimi nyumbani siku hiyo nikatoroka na nikarnda kumuona mama akiwa shamba fujoni.niliporudi nyumbani wakanipiga hapo nilikuwa kama miaka12 hawakujuwa lakini kama nilikuwa nimeenda kwa mama lakini kuna mtu mimi simjui nani alikuja kusema kuwa mimekweda kwa mama na walipojuwa kuwa nimekwnda kwa mama walinipiga pia na kunisimanga. toka siku hiyo nika siendi tena kwa mama sasa mimi ninamiaka 20 nishakuwa naakili sio kama ile ya zamani kila siku ya jumaapili ninakwenda kwa mama lakini natoroka sitaki wajue kwani wakijuwa itakuwa matatizo sana kwangu.na hata nikiwambia sasa hivi itakuwa kama ninampigia mbizi gitaa.sasa.

SASA NILIKUWA NATAKA USHAURI AU KAMA KUNA DUWA YA KUSOMA NIPENI NIPATE KUSOMA ILI WANIPERUHUSA NIPATE NIIJUWE FAMILA YA UPANDE WA MAMA.KWANI NI HAMU SANA YA KUIJUWA FAMILA YA UPANDE WA MAMA.NA KIWA SUBIRI WAO WANIPE RUHUSA NAONA NITACHELEWA SANA KUWASUBIRI.

NAOMBA MINIJIBU HARAKA KWANI NINA KAA KILA SIKU NA MAJOZI LINI NITAKAA NA MAMA NARUDIA TENA KAMA KUNA DUWA YA KUSOMA NAOMBA MUNIPE.

RAMAHDANI NJEMA.

Muulizaji amerudia kutuma tena Swali:

 

MIMI NILIKUWA NATAKA USHAURI KWANI MIMI KILA SIKU NAKUWA NAKAA KWA KUMUWAZA MAMA. SASA KAMA KUNA DAWA AU DUA YA KUSOMA NILIKUWA NATAKA MUNIPE KWANI MIMI WAZAZI WANGU WA UPANDE WA BABA HAWATAKI MIMI NIENDE UPANDE WA MAMA SASA MIMI NIFANYE NINI ILI WAWEZE KUNIPA RUHUSA NIENDE KWA MAMA.

SASA NILIKUWA NATA MUNIPE IYO DUA AU DAWA YA ILI NIPATE MIMI KUKAA NA MAMA

NAOM,BA MUNIJIBU HARAKA

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema anastahiki Allah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Kwanza tuwe

Hapana dawa ya shughuli hiyo na anayekwambia ipo basi kakudanganya. Iliyopo ni Da‘wah (kulingania) kwa wazazi wako wa upande wa baba. Unatakiwa ukae nao na uwaeleze namna Uislamu unavyomhimiza Muislamu kuwatendea wema wazazi wake na hasa mama yake. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipoulizwa:

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: جاء رجل إلى رسول الله صلى الله عليه وسلم فقال: يا رسول الله من أحق الناس بحسن صحابتي؟ قال:   (( أمك)) قال: ثم من؟ قال : (( أمك))

قال: ثم من؟ قال : (( أمك))  قال: ثم من؟ قال : ((أبوك))  رواه البخاري   ومسلم    

 

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allahu 'anhu) kwamba alikuja mtu kwa Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamuuliza: "Ewe Mjume wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala), nani mwenye haki zaidi mimi kumfanyia wema?". Akasema: ((Mama yako)) Kisha kasema: "Nani baada yake?" Akasema ((Mama yako))  Kisha kasema: "Nani baada yake?"   Akasema ((Mama yako)). Kisha kasema: "Nani baada yake?" Akasema: ((Baba yako)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Amekemea sana jambo hili la kukatisha mawasiliano ya wazazi na waliohusiana kwa damu hadi kufika kumlaani mwenye kufanya hivyo:

فَهَلْ عَسَيْتُمْ إِن تَوَلَّيْتُمْ أَن تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَتُقَطِّعُوا أَرْحَامَكُمْ

 

   أُوْلَئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّهُ فَأَصَمَّهُمْ وَأَعْمَى أَبْصَارَهُمْ  

 

((Basi yanayotarajiwa kwenu mkitawala ndio mfisidi katika nchi na muwatupe jamaa zenu))

((Hao ndio Allah Aliowalaani, na akawatia uziwi, na akawapofoa macho yao)) [Muhammad: 22-23]

((الَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهْدَ اللَّهِ مِن بَعْدِ مِيثَاقِهِ وَيَقْطَعُونَ مَا أَمَرَ اللَّهُ بِهِ أَن يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِي الأَرْضِ أُولَئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ))

 

((Wanaovunja ahadi ya Allah baada ya kwishaifunga, na wakayakata Aliyoamrisha Allah kuungwa, na wakafanya uharibifu katika nchi; hao ndio wenye khasara)) [Al-Baqarah:27]

 

Amesema Ibn Kathiry: Hii ina maana kukata uhusiano na jamaa na udugu kama alivyokiri Qataadah

Vile vile Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametukataza jambo hili katika Hadiyth nyingi, moja ifuatayo:

 

 عن أبي هريرة رضي الله عنه ان النبي صلى الله عليه وسلم قال : ((من كان يؤمن بالله واليوم الأخر فليصل رحمه )) رواه البخاري

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mwenye kumuamini Allah na siku ya Akhera, basi aungane na jamaa (udugu wa damu) zake)) [Al-Bukhaariy]

 

Kisha naye kakemea kuwa kukata udugu kutamharimisha mtu Pepo:

 قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:  (( لا يدخل الجنة قاطع رحم)) رواه الترمذي.

Amesema Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Haingii Peponi mwenye kukata udugu)) [At-Trimidhiy]

 

Ikiwa umeshindwa kuwakinaisha wazazi wako wa upande wa baba kukuruhusu kumtembelea mama yako, basi watumie    Mashaykh ambao wanaweza kuzungumza nao na kuwafahamisha umuhimu wa kuunga kizazi. Hii ni njia moja ambayo tunatarajia inaweza kuleta natija nzuri.

 

Njia nyengine ni kuinuka usiku na uswali Swalah ya usiku. Baada ya Swalah umuombe Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) Awalainishe nyoyo za wazazi wako hao. Bila shaka yoyote Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atakutolea njia katika hiyo shida na tatizo lako.

 

Hili lililokupata ni janga au balaa ya kutoweza kumuona au kumtembelea mama yako, hivyo Mtume (Swalla Llaahu 'alayhi wa sallam) anatutaka tuwe ni wenye kuomba dua hii hapa ili atuepushie na balaa hiyo.

لا إلَهَ إلاَّ اللَّهُ الْعَظـيمُ الْحَلِـيمْ، لا إلَهَ إلاَّ اللَّهُ   رَبُّ العَـرْشِ العَظِيـمِ، لا إلَهَ إلاَّ اللَّهُ  رَبُّ السَّمَـوّاتِ ورّبُّ الأَرْضِ ورَبُّ العَرْشِ الكَـريم

 

 Laa ilaha illaa Llahul ‘Adhiimul Haliim. Laa ilaha illaa Llaahu Rabbul ‘Arshil ‘Adhiim. Laa ilaha illaa Llahu Rabbus samawaati wa Rabbul ardhi wa Rabbul ‘Arshil Kariym”

“Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu  aliye Mtukufu Mpole, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu  Mola wa ‘Arshi  tukufu, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni  Mwenyezi Mungu  Mola wa mbingu na Mola wa ardhi na Mola wa ‘Arshi tukufu" (Al-Bukhaariy na Muslim).

 

Tunakuombea kwa Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) Akusahilishie na akuondolee tatizo hilo ili uweze kwenda na kumtazama mama yako na mwish muweze kukaa na kuishi pamoja naye inshaAllah.

Na Allah Anajua zaidi  

 

Share