18-Wewe Pekee Tunakuabudu: Tawassul Zinazokubalika: Kutawassal Kwa Aayah Katika Suwrah Az-Zumar
إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ
Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada
Tawassul Zinazokubalika
18-Kutawassa Kwa Aayah Katika Suwrah Az-Zumar
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
قُلِ اللَّـهُمَّ فَاطِرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ عَالِمَ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ أَنتَ تَحْكُمُ بَيْنَ عِبَادِكَ فِي مَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ﴿٤٦﴾
Sema: “Ee Allaah Muanzilishi wa mbingu na ardhi, Mjuzi wa ghayb na dhahiri, Wewe Utahukumu baina ya waja Wako katika ambayo walikuwa wakikhitilafiana nayo.” [Az-Zumar: 46]
Dalili ni Hadiyth ifautayo pamoja na kauli ya Sa’iyd bin Jubayr (Rahimahu Allaah) ambaye alikuwa ni miongoni mwa Taabi’uwn (waliofuatia baada ya Maswahaba):
عن أَبِي سَلَمَة بْن عَبْد الرَّحْمَن بْن عَوْف (رضي الله عنه) قَالَ: سَأَلْت عَائِشَة (رَضِيَ اللَّه عَنْهَا) بِأَيِّ شَيْء كَانَ النَّبِيّ (صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) يَسْتَفْتِح صَلاَته إِذَا قَامَ مِنْ اللَّيْل؟ قَالَتْ: كَانَ إِذَا قَامَ مِنْ اللَّيْل اِفْتَتَحَ صَلاَته ((اللَّهُمَّ رَبَّ جَبْرَائِيلَ وَمِيكَائِيلَ وَإِسْرَافِيلَ. فَاطِرَ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ. عَالِمَ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ. أَنْتَ تَحْكُمُ بَيْنَ عِبَادِكَ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ. اهْدِنِي لِمَا اخْتُلِفَ فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بِإِذْنِكَ إِنَّكَ تَهْدِي مَنْ تَشَاءُ إِلَى صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ).
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Salamah bin ‘Abdir-Rahmaan bin ‘Awf (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Nilimuuliza ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Je, Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akifungulia Swalaah yake kwa kitu gani alipoamka usiku? Akasema: alikuwa anapoamka usiku anafungulia Swalaah yake kwa:
اللَّهُمَّ رَبَّ جَبْرَائِيلَ وَمِيكَائِيلَ وَإِسْرَافِيلَ. فَاطِرَ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ. عَالِمَ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ. أَنْتَ تَحْكُمُ بَيْنَ عِبَادِكَ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ. اهْدِنِي لِمَا اخْتُلِفَ فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بِإِذْنِكَ إِنَّكَ تَهْدِي مَنْ تَشَاءُ إِلَى صِرَاطٍ مُسْتَقِيم
((Allaahumma Rabba Jibraaiyla wa Mikaaiyla wa Israafiyla, Faatwiras-samaawaati wal ardhw, ’Aalimal ghaybi wash-shahaadah, Anta Tahkmu bayna ’ibaadika fiymaa kaanuw fiyhi yakhtalifuwn. Ihdiniy limakhtulifa fiyhi minal haqqi biidhnika Innaka Tahdiy man Tashaau ilaa swiraatwil-mustaqiym –
Ee Allaah Rabb wa Jibraaiyl na Miykaaila na Israafiyla, Muanzilishi wa mbingu na ardhi, Mjuzi wa ghayb na dhahiri, Wewe Utahukumu baina ya waja Wako katika ambayo walikuwa wakikhitilafiana nayo. Niongoze mimi kwenye haki katika yale ambayo (watu) wamekhitilafiana kwa idhini Yako. Hakika Wewe unamuongoza Umtakae kwenye njia ilionyoka)). [Muslim (1/534)]
Na akasema Sa’iyd bin Jubayr:
إِنِّي لأَعْرِفُ آيَة مَا قَرَأَهَا أَحَد قَطُّ فَسَأَلَ اللَّه شَيْئًا إلاَّ أَعْطَاهُ إِيَّاهُ, قَوْله تَعَالَى: (( قُلِ اللَّـهُمَّ فَاطِرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ عَالِمَ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ أَنتَ تَحْكُمُ بَيْنَ عِبَادِكَ فِي مَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ))
“Hakika mimi ninaijua Aayah, haisomi mtu yeyote akamwomba Allaah kitu ila Anampa. Nayo ni kauli ya Allaah (Ta’aalaa): Sema: “Ee Allaah Muanzilishi wa mbingu na ardhi, Mjuzi wa ghayb na dhahiri, Wewe Utahukumu baina ya waja Wako katika ambayo walikuwa wakikhitilafiana nayo.” [Tafsiyr Al-Qurtwuby]