04-Kitaab At-Tawhiyd: Kukhofia Shirki
Mlango Wa 4
بَابُ الْخَوْفِ مِنْ اَلشِّرْكِ
Kukhofia Shirki
وَقَوْلِ اَللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ:
Na kauli Yake ‘Azza wa Jalla:
إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدِ افْتَرَىٰ إِثْمًا عَظِيمًا ﴿٤٨﴾
((Hakika Allaah Haghufuri kushirikishwa; lakini Anaghufuria yasiyokuwa hayo kwa Amtakae)) [An-Nisaa (4: 48, 116)]
وَقَالَ الْخَلِيلُ عَلَيْهِ اَلسَّلامُ :
Na amesema Khaliyl (Ibraahiym (عليه السلام:
وَاجْنُبْنِي وَبَنِيَّ أَن نَّعْبُدَ الْأَصْنَامَ ﴿٣٥﴾
((na Uniepushe na wanangu kuabudu masanamu)) [Ibraahiym (14: 35)]
وَفِي الْحَدِيثِ: ((أَخْوَفُ مَا أَخَافُ عَلَيْكُمْ اَلشِّرْكُ الأَصْغَرُ)) فَسُئِلَ عَنْهُ فَقَالَ: ((اَلرِّيَاءُ))
Na katika Hadiyth: ((Nnachokukhofieni zaidi juu yenu ni shirki ndogo)) Akaulizwa kuhusu hiyo shirki akasema: ((Riyaa)) [Ahmad katika Musnad yake (429, 428/5)]
وَعَنْ اِبْنِ مَسْعُودٍ (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ) أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((مَنْ مَاتَ وَهُوَ يَدْعُو مِنْ دُونِ اَللَّهِ نِدًّا دَخَلَ اَلنَّارَ)) رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ.
Na Imepokelewa kwa Ibn Mas’uwd(رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Yeyote atakayekufa hali anamshirikisha Allaah ataingia Motoni)) [Al-Bukhaariy]
وَلِمُسْلِمٍ عَنْ جَابِرٍ (رضي الله عنه) أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((مَنْ لَقِيَ اَللَّهَ لاَ يُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا, دَخَلَ الْجَنَّةَ. وَمَنْ لَقِيَهُ يُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا; دَخَلَ اَلنَّارَ))
Na kwa Muslim Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Atakayekutana na Allaah hali hamshirikishi na chochote ataingia Jannah. Na atakayekutana Naye hali anamshirikisha na chochote ataingia motoni)) [Muslim (93)]
Masuala Muhimu Yaliyomo:
1-Kukhofia shirki.
2-Riyaa ni aina ya shirki.
3-Riyaa ni shirki ndogo.
4-Riyaa inakhofiwa sana na waja wema (kwani rahisi mno mtu kutumbukia ndani yake)
5-Ukaribu wa Jannah na moto.
6-Ukaribu huo wa Jannah na Moto umetajwa katika Hadiyth moja.
7-Mwenye kukutana na Allaah (Siku ya Qiyaamah) akiwa hakumshirikisha na chochote ataingia Jannah; na mwenye kukutana Naye, huku amemshirikisha na kitu, ataingia motoni, hata kama alikuwa ni miongoni mwa wanaomwabudu mno Allaah (سبحانه وتعالى).
8-Umuhimu mkubwa mno wa suala hili, kiasi kwamba Al-Khaliyll (Ibraahiym) aliomba yeye na wanawe waepushwe dhidi ya kuabudu masanamu.
9-Kuzingatia kwake jinsi watu wengi walivyoingia katika ibaadah ya masanamu pindi aliposema:
رَبِّ إِنَّهُنَّ أَضْلَلْنَ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ
((“Rabb wangu! Hakika hao (masanamu) wamepoteza wengi sana katika watu)) [Ibraahiym (14:36)]
10-Tafsiri ya maana ya (kauli ya) “Laa ilaaha illaa Allaah” kama alivyoitaja Al-Bukhaariy.
11-Fadhila za aliyesalimika na shirki.