03-Kitaab At-Tawhiyd: Atakayethibitisha Tawhiyd (Dhidi ya Shirki) Ataingia Jannah Bila Ya Hesabu
Mlango Wa 3
بَابٌ :مَنْ حَقَّقَ اَلتَّوْحِيدَ دَخَلَ الْجَنَّةَ بِغَيْرِ حِسَابٍ
Atakayethibitisha Tawhiyd (Dhidi ya Shirki) Ataingia
Jannah Bila Ya Hesabu
وَقَوْلُ اَللَّهِ تَعَالَى:
Na kauli Yake Ta’aalaa:
إِنَّ إِبْرَاهِيمَ كَانَ أُمَّةً قَانِتًا لِّلَّـهِ حَنِيفًا وَلَمْ يَكُ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٢٠﴾
((Hakika Ibraahiym alikuwa Imaam mtiifu kwa Allaah, aliyeelemea haki na wala hakuwa miongoni mwa washirikina)) [An-Nahl (16: 120)]
وَقَالَ:
Na Anasema:
وَالَّذِينَ هُم بِرَبِّهِمْ لَا يُشْرِكُونَ ﴿٥٩﴾
((Na wale ambao Rabb wao hawamshirikishi)) [Al-Muuminuun (23:59)]
وَعَنْ حُصَيْنِ بْنِ عَبْدِ اَلرَّحْمَنِ قَالَ: كُنْتُ عِنْدَ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ فَقَالَ: أَيُّكُمْ رَأَى الْكَوْكَبَ اَلَّذِي اِنْقَضَّ الْبَارِحَةَ؟ فَقُلْتُ أَنَا. ثُمَّ قُلْتُ: أَمَّا إِنِّي لَمْ أَكُنْ فِي صَلاةٍ وَلَكِنِّي لُدِغْتُ. قَالَ: فَمَا صَنَعْتَ؟ قُلْتُ: اِرْتَقَيْتُ. قَالَ: فَمَا حَمَلكَ عَلَى ذَلِكَ؟ قُلْتُ: حَدِيثٌ حَدَّثَنَاهُ اَلشَّعْبِيُّ. قَالَ: وَمَا حَدَّثَكُمْ؟ قُلْتُ: حَدَّثَنَا عَنْ بُرَيْدَةَ بْنِ الْحُصَيْبِ أَنَّهُ قَالَ: لاَ رُقْيَةَ إِلاَّ مِنْ عَيْنٍ أَوْ حُمَةٍ. قَالَ: قَدْ أَحْسَنَ مَنِ اِنْتَهَى إِلَى مَا سَمِعَ. وَلَكِنْ حَدَّثَنَا اِبْنُ عَبَّاسٍ عَنْ اَلنَّبِيِّ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) أَنَّهُ قَالَ: ((عُرِضَتْ عَلَيَّ الأُمَمُ فَرَأَيْتُ اَلنَّبِيَّ وَمَعَهُ اَلرَّهْطُ وَالنَّبِيَّ وَمَعَهُ اَلرَّجُلُ وَالرَّجُلاَنِ، وَالنَّبِيَّ وَلَيْسَ مَعَهُ أَحَدٌ، إِذْ رُفِعَ لِي سَوَادٌ عَظِيمٌ فَظَنَنْتُ أَنَّهُمْ أُمَّتِي، فَقِيلَ لِي هَذَا مُوسَى وَقَوْمُهُ، فَنَظَرْتُ فَإِذَا سَوَادٌ عَظِيمٌ، فَقِيلَ لِي هَذِهِ أُمَّتُكَ، وَمَعَهُمْ سَبْعُونَ أَلْفًا يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ بِغَيْرِ حِسَابٍ وَلاَ عَذَابٍ)) ثُمَّ نَهَضَ فَدَخَلَ مَنْزِلَهُ فَخَاضَ اَلنَّاسُ فِي أُولَئِكَ فَقَالَ بَعْضُهُمْ: فَلَعَلَّهُمْ اَلَّذِينَ صَحِبُوا رَسُولَ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) ، وَقَالَ بَعْضُهُمْ فَلَعَلَّهُمْ اَلَّذِينَ وُلِدُوا فِي الإِسْلامِ فَلَمْ يُشْرِكُوا بِاَللَّهِ شَيْئًا وَذَكَرُوا أَشْيَاءَ. فَخَرَجَ عَلَيْهِمْ رَسُولُ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فَأَخْبَرُوهُ فَقَالَ: ((هُمُ اَلَّذِينَ لاَ يَسْتَرْقُونَ وَلاَ يَكْتَوُونَ وَلاَ يَتَطَيَّرُونَ وَعَلَى رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ)) فَقَامَ عُكَّاشَةُ بْنُ مُحْصَنٍ فَقَالَ: اُدْعُ اَللَّهَ أَنْ يَجْعَلَنِي مِنْهُمْ. فَقَالَ: ((أَنْتَ مِنْهُمْ)) ثُمَّ قَامَ رَجُلٌ آخَرُ فَقَالَ: اُدْعُ اَللَّهَ أَنْ يَجْعَلَنِي مِنْهُمْ. فَقَالَ: ((سَبَقَكَ بِهَا عُكَّاشَةُ)) البخاري ومسلم
Huswayn bin ‘Abdir-Rahmaan amehadithia: Siku moja nilipokuwa na Sa’iyd bin Jubayr, aliuliza: “Nani miongoni mwenu aliyeona kimondo (nyota inayofukuza shaytwaan) jana usiku?” Nikajibu: “Mimi nimeiona.” Kisha nikaelezea kwamba sikuwa nikiswali wakati ule sababu nilidonelewa na nge mwenye sumu. Akasema: “Kisha ukafanya nini?” Nikajibu: “Nilifanya Ruqyah (kujitibu). Akauliza: “Kitu gani kimekupeleka ufanye hivyo?” Nikasema: “Ni Hadiyth niliyoisikia kutoka
kwa Ash-Sha’biyy.” Akauliza: “Amekuhadithieni nini Ash-Sha’biyy?” Nikajibu: “Ameripoti kutoka kwa Buraydah bin Al-Huswayb amesema kwamba Ruqyah hairuhusiwi isipokuwa kwa ajili ya kijicho na kudonelewa (na mdudu sumu).” (Sa’iyd bin Jubayr) akasema: “Amefanya vyema kukomea kwenye aliyosikia (yaani: kufanyia kazi jambo kwa ujuzi kinyume na ujahili). Lakini Ibn ‘Abbaas ametusimulia kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Ummah zote zilipitishwa mbele yangu, nikamuona Nabiy akiwa na kundi dogo la watu, na Nabiy akiwa na mtu mmoja au wawili, na Nabiy akiwa hana mtu yeyote. Kisha nikaoneshwa idadi kubwa ya watu niliodhania ni katika Ummah wangu, lakini nikaambiwa: Huyo ni Muwsaa na watu wake. Kisha nikatazama nikaona kundi kubwa ambalo nikaamibwa: Hawa ni watu wako, miongoni mwao ni watu elfu sabini watakaoingia Jannah bila hesabu wala adhabu)). Kisha akainuka kuingia nyumbani kwake (na nyuma yake) watu wakaanza kujadiliaina ni nani hao watakaoweza kuwa. Wengineo wakasema: “Labda ni Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).” Wengine wakasema: “Labda ni wale waliozaliwa katika Uislamu na hawakumshirikisha Allaah kwa chochote.” (Wakataja mengine kadhaa) Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akatoka na kuja na wakamwambia (waliyokuwa wakiyajadili). Akasema: ((Ni wale ambao wasiotafuta (kuommba) kufanyiwa Ruqyah, wala kujichoma chuma cha moto, wala hawaamini twiyaarah [itikadi ya mkosi au nuksi], bali wanamtegemea Rabb wao na kutawakali Kwake Pekee)) ‘Ukaashah bin Mihswan akasimama akasema: “Muombe Allaah niwe mmoja wao.” Akasema: ((Wewe ni mmoja wao)). Kisha mtu mwengine akasimama akasema: Muombe Allaah niwe mmoja wao (pia). Akasema: ((‘Ukaashah amekutangulia)) [Al-Bukhaariy (3410) Muslim (220)]
Masuala Muhimu Yaliyomo:
1-Watu hutofautiana katika yakini zao juu ya Tawhiyd.
2-Maana halisi ya kutekeleza Tawhiyd.
3-Allaah (سبحانه وتعالى) kumsifia Ibraahiym (عليه السلام) kwamba: “si miongoni mwa washirikina.”
4-Allaah (سبحانه وتعالى) kuwasifu waja wema (awliyaa[1]) kwa kusalimika na shirki.
5-Kuikwepa Ruqyah na kuchomwa chuma cha moto ni miongoni mwa sifa za Tawhiyd.
6-Tawakkul (kumtegemea Allaah) inajumuisha sifa hizi.
7-Maswahaba kutambua tawakkul, kwani walijua wasingeifikia hali hiyo pasina ‘amali njema.
8-Utashi wa Maswahaba kwa kutenda kila lililo la khayr.
9-Fadhila za ummah huu (wa Kiislamu) kwa wingi na ubora.
10-Idadi kubwa ya wafuasi Muwsaa (عليه السلام).
11-Kudhiirishwa Ummah zote mbele ya Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)
12-Kila Ummah utakusanywa peke yake pamoja na Nabiy wake.
13-Uchache wa waliotikia wito wa Rusuli.
14-Rusuli ambao hawakuwa na wafuasi watahudhuria mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى) peke yao Siku ya Qiyaamah.
15-Faida ya elimu hii; kuwa mtu asidanganyike kwa wingi au kukatishwa tamaa na uchache wa idadi ya watu.
16-Ruhusa ya Ruqyah kwa ajili ya kijicho au kudonolewa na chenye sumu.
17-Ujuzi wa kina wa Salaf kama inavyoonekana katika kauli. “Amefanya vyema kukomea kwenye aliyosikia…” Tambua kwamba Hadiyth ya kwanza haikinzani na ya pili.
18-Kujiepusha kwa Salaf kumsifu mtu bila ya kustahiki.
19-Kauli ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ((Wewe ni miongoni mwao)) ni alama ya Unabiy.
20-Fadhila za ‘Ukaashah (رضي الله عنه).
21-Kutumia al-ma’aaridhw (mafumbo, mifano - kutaja kauli isiyo dhahiri, au kielezo fulani cha kutolea tafsiri mbali mbali).
22-Khulqa njema za Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم).
[1] Walio karibu na Allaah (سبحانه وتعالى) na vipenzi Wake.