02-Kitaab At-Tawhiyd: Fadhila Za Tawhiyd Na Yanayofuta Madhambi

02-Mlango Wa 2

بَابُ فَضْلِ التَّوْحِيدِ وَمَا يُكَفَّرُ مِنَ الذُّنُوبِ

Fadhila Za Tawhiyd Na Yanayofuta Madhambi


 

وَقَوْلُ اللَّهِ تَعَالَى:

Na kauli ya Allaah Ta’aalaa:

 

 الَّذِينَ آمَنُوا وَلَمْ يَلْبِسُوا إِيمَانَهُم بِظُلْمٍ أُولَـٰئِكَ لَهُمُ الْأَمْنُ وَهُم مُّهْتَدُونَ ﴿٨٢﴾

((Wale walioamini na hawakuchanganya iymaan zao na dhulma; hao ndio watakaopata amani nao ndio walioongoka)) [Al-An’aam (6: 82)]

 

عَنْ عُبَادَةَ بْنِ الصَّامِتِ (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم) ((مَنْ شَهِدَ أَنْ لاَ إلَهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ، وَأَنَّ عِيسَى عَبْدُ اللهِ وَرَسُولُهُ وَكَلِمَتُهُ أَلْقَاهَا إِلَى مَرْيَمَ وَرُوحٌ مِنْهُ، وَالْجَنَّةَ حَقٌّ وَالنَّارَ حَقٌّ أَدْخَلَهُ اللهُ الْجَنَّةَ عَلَى مَا كَانَ مِنَ الْعَمَلِ))    

Imepokelewa kutoka kwa ‘Ubaadah bin Asw-Swaamit(رضي الله عنه)  kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Atakayeshuhudia kwamba: Laa ilaaha illa-Allaah (hapana Muabudiwa wa haki ila Allaah) Pekee, Hana mshirikia, na kwamba Muhammad ni mja Wake na Rasuli Wake, na kwamba ‘Iysaa ni mja wa Allaah na Rasuli Wake, na Neno Lake Alilolitia kwa Maryam na Roho [imeumbwa] kutoka Kwake, na kwamba Jannah ni haki, na moto ni haki, Allaah Atamuingiza Jannah kwa kiasi chochote cha ‘amali yake itakavyokuwa)) [Al-Bukhaariy (3435), Muslim (28), At-Tirmidhiy]

 

فِي حَدِيثِ عِتْبَانَ ((فَإِنَّ اللهَ حَرَّمَ عَلَى النَّارِ مَنْ قَالَ لاَ إلَهَ إِلاَّ اللهُ يَبْتَغِي بِذَلِكَ وَجْهَ اللهِ))

Katika Hadiyth iliyopokewa toka kwa ‘Itbaan (رضي الله عنه): ((Hakika Allaah Ameharamisha moto kwa anayesema: “laa ilaaha illa-Allaah”, akikusudia kutafuta Wajihi wa Allaah)) [Al-Bukhaariy (425), Muslim (33)] 

 

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرَيِّ (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) عَنْ رَسُولِ الله (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ ((قَالَ مُوسَى عَلَيْهِ السَّلامُ يَا رَبِّ! عَلِّمْنِي شَيْئًا أَذْكُرُكَ وَأَدْعُوكَ بِهِ. قَالَ: قُلْ يَا مُوسَى: لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللهُ.  قَالَ يَا رَبِّ! كُلُّ عِبَادِكَ يَقُولُونَ هَذَا. قَالَ: يَا مُوسَى،  لَوْ أَنَّ السَّمَوَاتِ السَّبْعَ وَعَامِرَهُنَّ غَيْرِي وَالأَرَضِينَ السَّبْعَ فِي كِفَّةٍ،  وَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللهُ فِي كِفَّةٍ، مَالَتْ بِهِنَّ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللهُ))  رَوَاهُ ابْنُ حِبَّانَ وَالْحَاكِمُ وَصَحَّحَهُ.

Amesimulia Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه):  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Muwsaa alisema: Ee Rabb wangu! Nifundishe kitu mahsusi kwangu ambacho kwacho nitakudhukuru na kukuomba duaa. (Allaah) Akasema: Ee Muwsaa!    Sema:

لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللهُ 

Laa ilaaha illa-Allaah.  

 

Muwsaa akasema: Ee Rabb wangu! Waja Wako wote wanasema hivi. (Allaah) Akasema: Ee Muwsaa, lau kama mbingu saba na kila kilichokuwemo isipokuwa Mimi, na ardhi saba zikiwekwa katika kiganja cha mizani, na laa ilaaha illa-Allaah ikawekwa katika kiganja kingine cha mizani, basi laa ilaaha illa-Allaah itazishinda hizo.[Ibn Hibaan, na Al-Haakim ameikiri kuwa ni Swahiyh]

 

 

وَلِلتِّرْمِذِيِّ وَحَسَّنَهُ، عَنْ أَنَسٍ (رضي الله عنه) قال: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) يَقُولُ: ((قَالَ اللهُ تَعَالَى يَا ابْنَ آدَمَ! لَوْ آتَيْتَنِي بِقُرَابِ الأَرْضِ خَطَايَا ثُمَّ لَقِيتَنِي لاَ تُشْرِكُ بِي شَيْئًا لأَتَيْتُكَ بِقُرَابِهَا مَغْفِرَةً))

Na kwa At-Tirmidhiy aliyoipa daraja ya Hasan, Imepokelewa kutoka kwa Anas (رضي الله عنه) amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Allaah Ta’aalaa Amesema: Ee bin Aadam! Lau ukinijia kwa dunia iliyojaa madhambi, kisha ukakutana Nami hunishirikishi na chochote, bila shaka Nitakujia kwa wingi wa maghfirah kama hayo)) [At-Tirmidhiy (3534) Ad-Daarimiy (2791), Ahmad 172/5)]

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

 

1-Ukunjufu wa fadhila na rahmah za Allaah (سبحانه وتعالى).

 

2-Jazaa nyingi Anazozilipa Allaah (سبحانه وتعالى) kwa ajili ya Tawhiyd.

 

3-Tawhiyd inafuta dhambi juu ya kuwa ina fadhila na thawabu. 

 

4-Tafsiri ya Aayah katika Suwrah Al-An’aam (82).

 

5-Zingatia nukta tano zilizopatikana katika Hadiyth ya ‘Ubaadah bin Asw-Swaamit (رضي الله عنه).

 

6-Unapounganisha nukta hizi, Hadiyth ya ‘Itbaan (رضي الله عنه) na zinayoifuatia (ya ‘Itbaan), basi maana ya Kalimah ‘Laa ilaaha illaa Allaah’ inakuwa dhahiri kabisa na kudhihirisha makosa ya walioghurika nayo.

 

7-Kuzingatia sharti liliomo katika Hadiyth ya ‘Itbaan (رضي الله عنه).

 

8-Rusuli (عليهم السلام) walikuwa na haja ya kutanabahisha fadhila za ‘Laa ilaaha illa-Allaah’.

 

9-Tanbihi muhimu kwa viumbe wote kutamka Kalimah ‘Laa ilaaha illa-Allaah’ ingawa wengi wanaoitamka mizani zao zitakuwa khafifu.

 

10-Dalili yathibitisha kuwa kuna ardhi saba kama ambavyo ziko mbingu saba.[1]

 

11-Mbingu na ardhi zimejaa viumbe.

 

12-Kuthibitisha Sifa za Allaah (سبحانه وتعالى) kinyume na madai ya   Ash’ariyyah[2].

 

13-Unapoifahamu Hadiyth ya Anas (رضي الله عنه), utaifahamu pia kauli katika Hadiyth ya ‘Itbaan (رضي الله عنه). ((Hakika Allaah Ameharamisha moto kwa anayesema: “laa ilaaha illa-Allaah”, akikusudia kutafuta Wajihi wa Allaah)) yaani kwa kuepuka shirki, si kwa kuitamka kwa ulimi tu.

 

14-Kutafakari na kuzingatia sifa zinazolingana baina ya ‘Iysaa (عليه السلام) na Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم).

 

15-Kutambua kuwa ‘Iysaa (عليه السلام) alipewa sifa mahususi kuwa aliumbwa kwa ‘Kalimatu-Allaah’ (neno la Allaah).

 

16-Kujua kwamba ‘Iysaa (عليه السلام) ni Ruwhun Minhu (roho Alioumba kwa amrisho kutoka Kwake).  

 

17-Kujua fadhila za iymaan huko Jannah na motoni.

 

18-Kutambua kauli ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ((… kwa kiasi chochote cha ‘amali yake itakavyokuwa)).

 

19-Kujua kuwa Al-Miyzaan (mizani) ina pande mbili (za kipimo cha kuliani na kushotoni).

 

20-Maana ya ‘Wajihi wa Allaah’.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

[1] Rejea Surat At-Twalaaq (65:12).

[2] Baadhi ya ‘Aqiydah ya Ash’ariyyah ni kuzigeuza Sifa za Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kuzifasiri vinginevyo kinyume na vile zilivyothibitishwa katika Qur-aan na Sunnah.

Share