12-Kitaab At-Tawhiyd: Kuweka Nadhiri Kwa Asiyekuwa Allaah Ni Shirki
Mlango Wa 12
بَابٌ مِنْ اَلشِّرْكِ اَلنَّذْرُ لِغَيْرِ اَللَّهِ
Kuweka Nadhiri Kwa Asiyekuwa Allaah Ni Shirki
وَقَوْلُ اَللَّهِ تَعَالَى:
Na kauli ya Allaah Ta’aalaa:
يُوفُونَ بِالنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْمًا كَانَ شَرُّهُ مُسْتَطِيرًا ﴿٧﴾
((Ambao) Wanatimiza nadhiri na wanaiogopa siku ambayo shari yake ni yenye kuenea kwa upana)) [Al-Insaan (76: 7)]
وَقَوْلُهُ:
Na kauli Yake:
وَمَا أَنفَقْتُم مِّن نَّفَقَةٍ أَوْ نَذَرْتُم مِّن نَّذْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُهُ ۗ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ ﴿٢٧٠﴾
((Na chochote mtoacho (kwa ajili ya Allaah) au mkiwekacho nadhiri, basi Allaah Anakijua. Na madhalimu hawana wa kuwanusuru)) [Al-Baqarah (2: 270)]
وفي الصحيح عن عائشة (رضي الله عنها) أن الرسول صلى الله عليه وسلم قال: ((مَنْ نَذَرَ أَنْ يطيعَ اللهَ فَلْيطعْه وَمَنْ نَذَرَ أَن يَعْصيَ اللهَ فَلاَ يَعْصِه))
Na katika Asw-Swahiyh: Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah (رضي الله عنها) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Atakayeweka nadhiri kumtii Allaah na amtii. Na atakayeweka nadhiri kumuasi Allaah asimuasi)) [Al-Bukhaariy]
Masuala Muhimu Yaliyomo:
1-Kutimizia nadhiri ni wajibu.
2-Ikiwa imethibitishwa kuwa nadhiri hiyo ni miongoni mwa ‘ibaadah za kumwabudu Allaah (سبحانه وتعالى), basi kumfanyia mwengine ni shirki.
3-Hairuhusiwi kutekeleza nadhiri katika maasi.