17-Kitaab At-Tawhiyd: Ash-Shafaa’ah – Uombezi

Mlango Wa 17

بَابُ اَلشَّفَاعَةِ

Ash-Shafaa’ah – Uombezi

 

 

وَقَوْلِ اَللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ:

Na kauli ya Allaah ‘Azza wa Jalla:

 

وَأَنذِرْ بِهِ الَّذِينَ يَخَافُونَ أَن يُحْشَرُوا إِلَىٰ رَبِّهِمْ ۙ لَيْسَ لَهُم مِّن دُونِهِ وَلِيٌّ وَلَا شَفِيعٌ

((Na waonye kwayo (Qur-aan) wale wanaokhofu ya kwamba watakusanywa kwa Rabb wao; hawana badala Yake mlinzi wala mwombezi)) [Al-An’aam (6: 51)]

وَقَوْلِهِ:

Na kauli Yake:

 

قُل لِّلَّـهِ الشَّفَاعَةُ جَمِيعًا ۖ لَّهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ ثُمَّ إِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٤٤﴾

((Sema: “Uombezi wote ni wa Allaah Pekee…”)) [Az-Zumar (39: 44)]

وَقَوْلِهِ:

Na kauli Yake:

 مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ

((Nani huyu ambaye anashufai mbele Yake bila ya idhini Yake))  [Al-Baqarah (2: 255)]

 

وَقَوْلِهِ:   

Na kauli Yake:

 

وَكَم مِّن مَّلَكٍ فِي السَّمَاوَاتِ لَا تُغْنِي شَفَاعَتُهُمْ شَيْئًا إِلَّا مِن بَعْدِ أَن يَأْذَنَ اللَّـهُ لِمَن يَشَاءُ وَيَرْضَىٰ ﴿٢٦﴾

((Na Malaika wangapi mbinguni haitowafaa kitu chochote uombezi wao isipokuwa baada ya kuwa Allaah Ametolea idhini kwa Amtakaye na Akaridhia)) [An-Najm (53: 26)]

 

وَقَوْلِهِ:

Na kauli Yake:

 

قُلِ ادْعُوا الَّذِينَ زَعَمْتُم مِّن دُونِ اللَّـهِ ۖ لَا يَمْلِكُونَ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ  

((Sema: “Ombeni wale mnaodai kwa dhana (ni waabudiwa) badala ya Allaah, hawamiliki hata uzito wa sisimizi mbinguni wala ardhini)) [Sabaa (34: 22)]

 

قَالَ أَبُو الْعَبَّاسِ، نَفَى اَللَّهُ عَمَّا سِوَاهُ كُلَّ مَا يَتَعَلَّقُ بِهِ الْمُشْرِكُونَ، فَنَفَى أَنْ يَكُونَ لِغَيْرِهِ مُلْكٌ أَوْ قِسْطٌ مِنْهُ أَوْ يَكُونَ عَوْنًا لِلَّهِ وَلَمْ يَبْقَ إِلاَّ اَلشَّفَاعَةُ، فَبَيَّنَ أَنَّهَا لاَ تَنْفَعُ إِلاَّ لِمَنْ أَذِنَ لَهُ اَلرَّبُّ، كَمَا قَالَ: ((وَلَا يَشْفَعُونَ إِلَّا لِمَنِ ارْتَضَىٰ ))

Abuu Al-‘Abbaas[1] amesema: “Allaah Amekanusha kila kisichokuwa Yeye ambacho washirikina wanawanyenyekea.  Akakanusha kuwa hakuna isipokuwa Yeye Allaah Mwenye milki na uwezo. Hakuna mwenye kusaidia ila Yeye. Kinachobaki ni shafaa’ah. Akabainisha kwamba hautomfaa yeyote isipokuwa ambaye amepewa idhini ya Rabb kama Anavyosema: ((na wala hawataomba shafaa’ah (yeyote) isipokuwa kwa yule ambaye (Allaah) Amemridhia)) [Al-Anbiyaa (21: 28)]

 

فَهَذِهِ اَلشَّفَاعَةُ اَلَّتِي يَظُنُّهَا الْمُشْرِكُونَ هِيَ مُنْتَفِيَةٌ يَوْمَ الْقِيَامَةِ، كَمَا نَفَاهَا الْقُرْآنُ، وَأَخْبَرَ اَلنَّبِيُّ  (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)  أَنَّهُ يَأْتِي فَيَسْجُدُ لِرَبِّهِ وَيَحْمَدُهُ  لاَ يَبْدَأُ بِالشَّفَاعَةِ أَوَّلاً - ثُمَّ يُقَالُ لَهُ اِرْفَعْ رَأْسَكَ وَقُلْ يُسْمَعْ وَسَلْ تُعْطَ وَاشْفَعْ تُشَفَّعْ.  

Kwa sababu hiyo shafaa’ah wanayoiamini washirikna itakanushwa Siku ya Qiyaamah kama ilivyokanushwa na Qur-aan na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliposema kwamba: Atafika kisha atamsujudia Rabb wake atamhimidi, na hatoanza kwanza kwa shafaa’ah. Kisha itasemwa: “Inua kichwa chako! Sema utasikilizwa! Omba utapewa! Omba shafaa’ah utaruhusiwa kuombeza)) [Al-Bukhaariy na Muslim]   

 

وَقَالَ لَهُ أَبُو هُرَيْرَةَ (رضي اَللَّهُ عَنْهُ): مَنْ أَسْعَدُ اَلنَّاسِ بِشَفَاعَتِكَ؟ قَالَ: ((مَنْ قَالَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اَللَّهُ خَالِصًا مِنْ قَلْبِهِ))

Abuu Hurayrah (رضي اَللَّهُ عَنْهُ) alimuuliza: “Nani atakayefanikiwa zaidi na shafaa’ah yako? Akajibu: ((Atakayesema Laa ilaaha illa-Allaah, hali ya kuwa na niyyah safi moyoni mwake)) [Al-Bukhaariy]

 

فَتِلْكَ اَلشَّفَاعَةُ لأَهْلِ الإِخْلاصِ بِإِذْنِ اَللَّهِ، وَلا تَكُونُ لِمَنْ أَشْرَكَ بِاَللَّهِ

Basi hiyo ndio shafaa’ah kwa watu wenye ikhlaasw kwa idhini ya Allaah, wala haitokuwa kwa anayemshirikisha Allaah.

 

وَحَقِيقَتُهُ أَنَّ اَللَّهَ سُبْحَانَهُ هُوَ اَلَّذِي يَتَفَضَّلُ عَلَى أَهْلِ الإِخْلاصِ، فَيَغْفِرُ لَهُمْ بِوَاسِطَةِ دُعَاءِ مَنْ أَذِنَ لَهُ أَنْ يَشْفَعَ، لِيُكْرِمَهُ وَيَنَالَ الْمَقَامَ الْمَحْمُودَ

Na uhakika wake (shafaa’ah hiyo) ni kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Ambaye Anayewafanyia ihsaan watu wa ikhlaasw [katika ‘ibaadah zao]. Atawaghufuria kwa wasita wa du’aa au shafaa’ah ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ili Amkirimu na aweze (صلى الله عليه وآله وسلم) kufikia cheo cha Al-Maqaam Al-Mahmuwd[2].   

 

فَالشَّفَاعَةُ اَلَّتِي نَفَاهَا الْقُرْآنُ مَا كَانَ فِيهَا شِرْكٌ، وَلِهَذَا أَثْبَتَ اَلشَّفَاعَةَ بِإِذْنِهِ فِي مَوَاضِعَ وَقَدْ بَيَّنَ اَلنَّبِيُّ  (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) أَنَّهَا لاَ تَكُونُ إِلاَّ لأَهْلِ الإِخْلاصِ وَالتَّوْحِيدِ.  اِنْتَهَى كَلامُهُ

Basi shafaa’ah inayokanushwa na Qur-aan ni iliyo na shirki, na ndio maana shafaa’ah imethibiti kwa idhini ya Allaah sehemu nyingi na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amebainisha kwamba shafaa’ah haitokuwa isipokuwa kwa watu wa Tawhiyd na ikhlaasw [katika Dini yao]” - Mwisho wa maneno ya Ibn Taymiyyah.

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Tafsiri ya Aayah zilizotajwa.

 

2-Maelezo ya aina ya shafaa’ah iliyokanushwa.

 

3-Maelezo ya aina ya shafaa’ah iliyothibiti.

 

4-Kutajwa shafaa’ah kuu (ya Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) na kuhusu Al-Maqaam Al-Mahmuwd.

 

5-Atakalofanya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), na kwamba hatoanza na shafaa’ah, bali atasujudu, halafu atakapopewa idhini ndipo atakapoinuka kuombea shafaa’ah.

 

6-Nani atakayefaidika kupata hadhi hiyo ya shafaa’ah ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)?

 

7-Shafaa’ah haitokuwa kwa wanaomshirikisha Allaah (سبحانه وتعالى).

 

8-Kubainisha ukweli wa shafaa’ah.

 

 

 

 

 

 

[1] Shaykhul-Islaam Taqiyyud-Diyn Ahmad bin ‘Abdil-Haliym bin ‘Abdis-Salaam, bin Taymiyyah - Fat-hul-Majiyd, uk. 168.

[2] Mahali pa kuhimidiwa katika cheo kikuu Jannah.

 

 

Share