18-Kitaab At-Tawhiyd: Hakika Wewe Huwezi Kumhidi Umpendaye

Mlango Wa 18

باب:  إِنَّكَ لَا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ

Hakika Wewe Huwezi Kumhidi Umpendaye


 

 

قَوْلُ اَللَّهِ تَعَالَى:

Kauli ya Allaah Ta’aalaa:

 

إِنَّكَ لَا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ ﴿٥٦﴾

((Hakika wewe huwezi kumhidi umpendaye; lakini Allaah Humhidi Amtakaye, Naye Anawajua zaidi wenye kuongoka)) [Al-Qaswasw (28: 56)]

 

وَفِي اَلصَّحِيحِ، عَنْ اِبْنِ الْمُسَيَّبِ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: لَمَّا حَضَرَتْ أَبَا طَالِبٍ الْوَفَاةُ; جَاءَهُ رَسُولُ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) وَعِنْدَهُ عَبْدُ اَللَّهِ بْنُ أَبِي أُمِّيَّةَ وَأَبُو جَهْلٍ فَقَالَ لَهُ: ((يَا عَمِّ قُلْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اَللَّهُ كَلِمَةً أُحَاجُّ لَكَ بِهَا عِنْدَ اَللَّهِ)) فَقَالاَ لَهُ: أَتَرْغَبُ عَنْ مِلَّةِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ؟ فَأَعَادَ عَلَيْهِ اَلنَّبِيُّ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فَأَعَادَا، فَكَانَ آخَرَ مَا قَالَ: هُوَ عَلَى مِلَّةِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ، وَأَبَى أَنْ يَقُولَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اَللَّهُ فَقَالَ اَلنَّبِيُّ  (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((لأَسْتَغْفِرَنَّ لَكَ مَا لَمْ أُنْهَ عَنْكَ)). فَأَنْزَلَ اَللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ: ((مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ)) وَأَنْزَلَ اَللَّهُ فِي أَبِي طَالِبٍ: ((إِنَّكَ لَا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ))

 

Katika Swahiyh, Ibn Musayyib amehadithia kutoka kwa baba yake: Mauti yalipomkaribia Abuu Twaalib, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimwendea akamkuta ‘Abdullaah bin Abiy Umayyah na Abuu Jahl wakiwa pamoja naye. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Ee ‘ammi wangu! Sema laa ilaaha illa-Allaah, hivyo utaniwezesha kukuombea shafaa’ah kwa Allaah)) Wawili hao wakamwambia: Utaacha dini ya [baba yako] ‘Abdul-Muttwalib? Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akakariri [ombi lake] na wawili hao wakakariri nao vile vile. Ikawa neno la mwisho alosema ni kubakika katika dini ya ‘Abdul-Muttwalib. Akafariki akiwa amekataa kusema ‘laa ilaaha illa-Allaah’. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Nitaendelea kukuombea maghfirah madamu sijakatazwa kufanya hivyo)). Hapo Allaah ‘Azza wa Jalla Akateremsha Aayah: ((Haimpasi Nabiy na wale walioamini kuwaombea maghfirah washirikina japokuwa ni jamaa zao wa karibu)) [At-Tawbah (9: 113)] Kisha Akateremsha kuhusu Abuu Twaalib: ((Hakika wewe huwezi kumhidi umpendaye; lakini Allaah Humhidi Amtakaye, Naye Anawajua zaidi wenye kuongoka)) [Al-Qaswasw (28: 56)]

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Tafsiri ya Aayah katika Suwrah Al-Qaswasw (28: 56)

إِنَّكَ لَا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ

((Hakika wewe huwezi kumhidi umpendaye; lakini Allaah Humhidi Amtakaye)).

 

2-Tafsiri ya Aayah:

 

مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ ﴿١١٣﴾

((Haimpasi Nabiy na wale walioamini kuwaombea maghfirah washirikina japokuwa ni jamaa zao wa karibu baada ya kuwabainikia kwamba wao ni watu wa moto uwakao vikali mno)) [At-Tawbah (9: 113)].

 

3-Suala kubwa la tafsiri ya kauli yake (صلى الله عليه وآله وسلم): ((Sema, Laa ilaaha illaa Allaah)) Inakinzana na madai ya wanodai kuwa wana ujuzi wa elimu ya Dini (kudai kwao kwamba kuitamka kwake inatosheleza kusamehewa juu ya kwamba wanawaomba na kuwaabudu mawalii wao). 

 

4-Abuu Jahl na wenzake walijua kusudio la Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipomwambia Abuu Twaalib: ((Sema ‘Laa ilaaha illaa Allaah)), Basi Allaah (سبحانه وتعالى) Amdhalilishe yeyote ambaye elimu yake juu ya asili ya Uislamu ni ndogo kuliko ile ya Abuu Jahl.   

 

5-Hima utashi wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kumsilimisha ‘ammi yake.

 

6-Kukanushwa yeyote anayedai kuwa ‘Abdul-Muttwalib na baba zake walikuwa Waislamu.

 

7-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimwombea ‘ammi yake msamaha lakini hakusamehewa, na kuwa hilo limekatazwa.

 

8-Madhara ya kuandamana na waovu.

 

9-Madhara ya kuwatukuza kibubusa viongozi na wahenga (na hali ni washirikina).

 

10-Shubuha za wapotofu katika hilo ni hoja za ujaahiliyyah (kama Abuu Jahl alivyojitokeza).

 

11-Dalili kwamba ‘amali za mmojawapo zinategemea mwisho wake, kwa sababu kama angeitamka laa ilaaha illa-Allaah, angeliokoka.

 

12-Zingatio la hoja hii ya mwisho katika nyoyo za wapotofu kujivunia dini na mila za mababu, kwa sababu kisa kinathibitisha kwamba hawakujadiliana naye isipokuwa kuhusu kuing’ang’ania dini au mila zao, japokuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliendelea kumbembeleza Abuu Twaalib atamke shahaada, kwani angelishuhudia angeliokoka, lakini wao wakashikilia tu umuhimu wa kufuata dini ya wazazi wao.

 

 

 

Share