19-Kitaab At-Tawhiyd: Sababu WanaAadam Kukufuru, Kuacha Dini Kupinduka Mipaka Kutukuza Waja Wema

Mlango Wa 19

بَابُ مَا جَاءَ أَنَّ سَبَبَ كُفْرِ بَنِي آدَمَ وَتَرْكِهِمْ دِينَهُمْ هُوَ الْغُلُوُّ فِي اَلصَّالِحِينَ

Sababu Ya Wana Aadam Kukufuru Na kuacha Dini Yao Ni Kupindukia Mipaka Katika Kuwatukuza Waja Wema


 

 

وَقَوْلِ اَللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ:  

 Na kauli ya Allaah ‘Azza wa Jalla:

 يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لَا تَغْلُوا فِي دِينِكُمْ

((Enyi Ahlal-Kitaabi! Msipindukie mipaka katika dini yenu)) [An-Nisaa (4: 171)]

 

وَفِي اَلصَّحِيحِ عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا) فِي قَوْلِ اَللَّهِ تَعَالَى: ((وَقَالُوا لَا تَذَرُنَّ آلِهَتَكُمْ وَلَا تَذَرُنَّ وَدًّا وَلَا سُوَاعًا وَلَا يَغُوثَ وَيَعُوقَ وَنَسْرًا )) قَالَ: ((هَذِهِ أَسْمَاءُ رِجَالٍ صَالِحِينَ مِنْ قَوْمٍ نُوحٍ ، فَلَمَّا هَلَكُوا أَوْحَى اَلشَّيْطَانُ إِلَى قَوْمِهِمْ أَنِ انْصُبُوا إِلَى مَجَالِسِهِمْ اَلَّتِي كَانُوا يَجْلِسُونَ فِيهَا أَنْصَابًا وَسَمُّوهَا بِأَسْمَائِهِمْ، فَفَعَلُوا وَلَمْ تُعْبَدْ حَتَّى إِذَا هَلَكَ أُولَئِكَ وَنُسِيَ الْعِلْمُ عُبِدَتْ))

Na katika Swahiyh Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا) amesema kuhusu kauli ya Allaah Ta’aalaa: ((Wakasema: “Msiwaache waabudiwa wenu; na wala msimwache Waddaa, na wala Su’waa’a, na wala Yaghuwtha, na Ya’uwqa, na Nasraa)) [Nuwh (71: 23)] Akasema: ((Haya ni majina ya waja wema miongoni mwa kaumu ya Nuwh. Walipofariki shaytwaan aliwashawishi watu wawaweke kama masanamu kuwaheshimu na wakawaweka katika mabaraza yao waliyokuwa wakikaa. Wakawaita majina yao hao waja wema waliofariki. Hapo mwanzoni hawakuwa wakiwaabudu, hadi watu hao walipofariki, na iliposahauliwa asili yake masanamu hayo yakaanza kuabudiwa))

 

قَالَ اِبْنُ الْقَيِّمِ:  قَالَ غَيْرُ وَاحِدٍ مِنْ اَلسَّلَفِ: لَمَّا مَاتُوا، عَكَفُوا عَلَى قُبُورِهِمْ، ثُمَّ صَوَّرُوا تَمَاثِيلَهُمْ ثُمَّ طَالَ عَلَيْهِمْ الأَمَدُ فَعَبَدُوهُمْ

Ibn Al-Qayyim  (رحمه الله)amesema: “Aghlabu ya As-Salaf wamesema: “Baada ya kufariki (waja wema) wakawawekea mipaka makaburini mwao na wakaweka masanamu yao na baada ya muda kupita wakaanza kuyaabudu.”

 

وَعَنْ عُمَرَ (رضي الله عنه): أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((لاَ تُطْرُونِي كَمَا أَطْرَتِ اَلنَّصَارَى اِبْنَ مَرْيَمَ، إِنَّمَا أَنَا عَبْدٌ، فَقُولُوا عَبْدُ اَللَّهِ وَرَسُولُهُ)) أَخْرِجَاهُ

Imepokelewa kutoka kwa ‘Umar bin Al-Khattwaab (رضي الله عنه)  kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Msinitukuze kama Manaswara walivyomtukuza  mwana wa Maryam, hakika mimi ni mja kwa hiyo semeni mja wa Allaah na Rasuli Wake)) [Al-Bukhaariy na Muslim]   

 

وقَالَ رَسُولُ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)): ((إِيَّاكُمْ وَالْغُلُوَّ فَإِنَّمَا أَهْلَكَ مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ الْغُلُوُّ))

Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Tahadharini na upindukiaji mipaka ya Dini, kwani waliokuwa kabla yenu waliangamia kwa sababu ya uvukaji mipaka ya Dini)) [Ahmad, An-Nasaaiy, Ibn Maajah, Ibn Khuzaymah, Al-Haakim na Adh-Dhahabiy kaiwafiki kuwa ni Swahiyh]

 

 وَلِمُسْلِمٍ عَنْ اِبْنِ مَسْعُودٍ  (رضي الله عنه) أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)  قَال:  ((هَلَكَ الْمُتَنَطِّعُونَ))  قَالَهَا ثَلَاثًا

Na (Swahiyh) Muslim amepokea kutoka kwa Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Wameangamia wapindukiaji mipaka)) amesema mara tatu. [Muslim]

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Yeyote anayeelewa mlango huu hii na miwili inayofuatia, atadhihirikiwa upekee wa Uislamu na atafahamu Qudra ya Allaah (سبحانه وتعالى) ya kuzibadlisha nyoyo.

 

2-Kujua kuwa shirki ya kwanza kabisa ilyozuka duniani ilihusu waja wema (kudhania wana sifa na uwezo kama wa Allaah).

 

3-Jambo la kwanza kubadilishwa katika dini ya Rusuli na kilichosababisha hivyo, juu ya kujulikana kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye aliyewatuma.

 

4-Kutambua sababu ya kuikubali bid’ah licha ya kuwa ni kinyume na Shariy’ah (ya Dini) na maumbile.

 

5-Sababu ya yote haya ni kuchanganya haki na batili. Mwanzo ilikuwa kuwatukuza waja wema. La pili ni baadhi ya watu wa elimu walikuwa walikifanya kwa niyyah njema, lakini vizazi vilivyokuja baadaye walikusudia vinginevyo.

 

6-Tafsiri ya Aayah katika Suwratun-Nuwh (71: 23)

 

7-Maumbile ya mwana Aadam, haki hupungua moyoni mwake, na hapo upotofu huongezeka (isipokuwa ambaye Allaah (سبحانه وتعالى) Amemteremshia rahmah Yake).

 

8-Inathibitisha kauli za Salaf kuwa bid’ah ni sababu ya kufr, nayo inapendwa mno na Ibliys kuliko maasi, kwa sababu mtu hutubia maasi, ama bid’ah hatubii (kwa kuwa anadhania ni ‘amali njema). 

 

9-Ufahamu wa shaytwaan wa natija ya mwisho kuhusu bid’ah inavyopelekea (katika upotofu) hata kama niyyah ya mtu ilikuwa ni safi. 

 

10-Kujifunza kanuni ya kijumla nayo ni kukatazwa kupindukia mipaka na kufahamu inapelekea wapi. 

 

11-Madhara ya ziara ndefu makaburini hata ikiwa ni kwa niyyah ya kufanya ‘amali njema.

 

12-Kukatazwa masanamu na hekima ya kuyavunjulia mbali.

 

13-Kujua umuhimu wa kisa hiki, na kusisitiza kupata mafunzo yake na kutokughafilika nacho kwa kuwa ni jambo linalopuuzwa.

 

14-Ni ajabu kubwa, wanalisoma hilo katika vitabu vya Tafsiyr na Hadiyth, na wanaelewa maana yake, lakini juu ya hivyo, Allaah (سبحانه وتعالى) Ameziwekea vikwazo nyoyo zao hadi wakaitakidi kuwa matendo ya kaumu Nuwh (kuwatukuza waja wema waliofariki na makaburi yao) ni aina bora ya ‘ibaadah na wakaamini Alivyovikataza Allaah (سبحانه وتعالى) na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) ni kufru inayohalalisha damu na mali ya wakanushao.

 

15-Ufafanuzi kuwa wao kwa matendo yao walikusudia shafaa’ah tu.

 

16-Waliamini kuwa wenye elimu waliochonga masanamu walikuwa na niyyah hiyo hiyo.

 

17-Ufafanuzi wa kauli yake: ((Msinitukuze kama Manaswara walivyomtukuza mwana wa Maryam)). Allaah Amshushie rahmah na amani kwa kubalighisha ujumbe wake waziwazi.

 

18-Onyo lake kwetu kwamba kupindukia mipaka ya Dini inapeleka katika maangamizi.

 

19-Maelezo kwamba masanamu hayakuabudiwa isipokuwa baada ya elimu ya asili yake kupotea. Hii inatambulisha thamani ya elimu ya historia na madhara ya kukosekana kwake.

 

20-Sababu ya kupotea elimu ni kufariki kwa Wanachuoni.

 

 

 

 

Share