20-Kitaab At-Tawhiyd: Haramisho La Kumwabudu Allaah Kwenye Kaburi La Mja Mwema
Mlango Wa 20
بَابُ مَا جَاءَ مِنْ اَلتَّغْلِيظِ فِيمَنْ عَبَدَ اَللَّهَ عِنْدَ قَبْرِ رَجُلٍ صَالِحٍ، فَكَيْفَ إِذَا عَبَدَهُ؟
Kushadidishwa Haramisho La Kumwabudu Allaah Kwenye Kaburi La Mja Mwema, Basi Ubaya Ulioje Akimuabudu Huyo Mja Mwema?
فِي اَلصَّحِيحِ عَنْ عَائِشَةَ (رضي الله عنها) أَنَّ أُمَّ سَلَمَةَ ذَكَرَتْ لِرَسُولِ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) كَنِيسَةً رَأَتْهَا بِأَرْضِ الْحَبَشَةِ، وَمَا فِيهَا مِنْ اَلصُّوَرِ فَقَالَ: ((أُولَئِكَ إِذَا مَاتَ فِيهِمْ اَلرَّجُلُ اَلصَّالِحُ أَوْ الْعَبْدُ اَلصَّالِحُ، بَنَوْا عَلَى قَبْرِهِ مَسْجِدًا، وَصَوَّرُوا فِيهِ تِلْكَ اَلصُّوَرَ، أُولَئِكَ شِرَارُ الْخَلْقِ عِنْدَ اَللَّهِ. فَهَؤُلاءِ جَمَعُوا بَيْنَ الْفِتْنَتَيْنِ فِتْنَةَ الْقُبُورِ، وَفِتْنَةَ اَلتَّمَاثِيلِ))
Katika Swahiyh, Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah (رضي الله عنها) kwamba Ummu Salamah alimtajia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba aliona kanisa zuri Abyssinia lilojaa picha na masanamu. Akasema: ((Hao, anapokufa mtu mwema miongoni mwao, au mja mwema, hujenga Msikiti juu ya kaburi lake. Kisha wakazichora ndani yake picha hizo. Hao ni viumbe waovu mbele ya Allaah. Basi hao wamejumuisha baina ya fitnah mbili; fitnah ya makaburi na fitnah ya masanamu)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
وَلَهُمَا عَنْهَا، قَالَتْ: لَمَّا نَزَلَ بِرَسُولِ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)) طَفِقَ يَطْرَحُ خَمِيصَةً لَهُ عَلَى وَجْهِهِ، فَإِذَا اِغْتَمَّ بِهَا كَشَفَهَا فَقَالَ وَهُوَ كَذَلِكَ: ((لَعْنَةُ اَللَّهُ عَلَى الْيَهُودِ وَالنَّصَارَى، اِتَّخَذُوا قُبُورَ أَنْبِيَائِهِمْ مَسَاجِدَ)) يُحَذِّرُ مَا صَنَعُوا، وَلَوْلاَ ذَلِكَ، أُبْرِزَ قَبْرُهُ، غَيْرَ أَنَّهُ خَشِيَ أَنْ يُتَّخَذَ مَسْجِدًا - أَخْرِجَاهُ
Na kutoka kwao pia, amesema ‘Aaishah (رضي الله عنها): Mauti yalipomkaribia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alianza kuchomoa kipande cha kitambaa [cha shuka ya kitanda] akijiwekea usoni mwake [mara akijifunika mara akijifunua kutokana na Sakaratul-Mawti]. Akasema alipokuwa katika hali hiyo: ((Allaah Awalaani Mayahudi na Manaswara kwa kufanya makaburi ya Manabii wao kuwa mahali pa ‘ibaadah)). Akawatahadharisha watu kuhusu vitendo vyao. Ingelikuwa si kuchelea hivyo [khofu ya kufanya kaburi la Nabiy kuwa mahali pa ‘ibaadah], basi kaburi lake lingeliwekwa wazi [kama yalivyowekwa wazi makaburi ya Maswahaba wake] [Al-Bukhaariy na Muslim]
وَلِمُسْلِمٍ عَنْ جُنْدُبِ بْنِ عَبْدِ اَللَّهِ قَالَ سَمِعْتُ اَلنَّبِيَّ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَبْلَ أَنْ يَمُوتَ بِخَمْسٍ وَهُوَ يَقُولُ: ((إِنِّي أَبْرَأُ إِلَى اَللَّهِ أَنْ يَكُونَ لِي مِنْكُمْ خَلِيلٌ فَإِنَّ اَللَّهَ قَدْ اِتَّخَذَنِي خَلِيلاً كَمَا اِتَّخَذَ إِبْرَاهِيمَ خَلِيلاً، وَلَوْ كُنْتُ مُتَّخِذًا مِنْ أُمَّتِي خَلِيلاً، لَاِتَّخَذْتُ أَبَا بَكْرٍ خَلِيلاً، أَلَا وَإِنَّ مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ كَانُوا يَتَّخِذُونَ قُبُورَ أَنْبِيَائِهِمْ مَسَاجِدَ، أَلَّا فَلَا تَتَّخِذُوا الْقُبُورَ مَسَاجِدَ، فَإِنِّي أَنْهَاكُمْ عَنْ ذَلِك))
Na Muslim kasimulia kutoka kwa Jundub bin ‘Abdullah (رضي الله عنه) amesema: Nilimsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema siku tano kabla ya kufariki kwake: ((Mimi sina hatia kwa Allaah kumfanya mmoja wenu kuwa khalili. Hakika Allaah Amenifanya mimi kuwa ni khalili Wake kama alivyomfanya Ibraahiym kuwa khalili. Ningekuwa wa kufanya khalili katika Ummah wangu, basi ningemfanya Abuu Bakr kuwa khalili wangu Tahadharini! Waliotangulia kabla yenu walikuwa wakifanya makaburi ya Manabii wao mahali pa ‘ibaadah. Tahadharini! Msifanye makaburi [yoyote] kuwa ni mahali pa ‘ibaadah nakukatazeni kufanya hivyo)) [Muslim]
فَقَدْ نَهَى عَنْهُ فِي آخِرِ حَيَاتِهِ، ثُمَّ إِنَّهُ لَعَنَ وَهُوَ فِي اَلسِّيَاقِ مَنْ فَعَلَهُ. وَالصَّلاةُ عِنْدَهَا مِنْ ذَلِكَ وَإِنْ لَمْ يُبْنَ مَسْجِدٌ.وَهُوَ مَعْنَى قَوْلِهِ: خُشِيَ أَنْ يُتَّخَذَ مَسْجِدًا. فَإِنَّ اَلصَّحَابَةَ لَمْ يَكُونُوا لِيَبْنُوا حَوْلَ قَبْرِهِ مَسْجِدًا. وَكُلُّ مَوْضِعٍ يُصَلَّى فِيهِ يُسَمَّى مَسْجِدًا كَمَا قَالَ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((جُعِلَتْ لِيَ الْأَرْضُ مَسْجِدًا وَطَهُورًا))
Amekataza hilo katika mwisho wa umri wake. Kisha (baada ya kukataza kufanya makaburi kuwa Misikiti, yaani mahali pa ‘ibaadah) akalaani yeyote atakayefanya kitendo hicho. Na kuswali makaburini ni sawa na kulifanya kaburi kuwa ni Msikiti hata kama hamna Msikiti uliojengwa hapo kaburini. Hii ndio maana ya kauli yake (صلى الله عليه وآله وسلم): ‘Khofu ya kufanya (kaburi lake) kuwa ni Msikiti’. Maswahaba hawajapato kujenga Msikiti kaburini mwake. Na kila mahali panaposwaliwa panaitwa ‘Masjid’ (Msikiti) kama alivyosema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): ((Ardhi imefanywa kwangu kuwa ni Masjid na mahali twahaarah)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
وَلأَحْمَدَ بِسَنَدٍ جَيِّدٍ عَنْ اِبْنِ مَسْعُودٍ (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ) مَرْفُوعًا: ((إِنَّ مِنْ شِرَارِ اَلنَّاسِ مَنْ تُدْرِكُهُمْ اَلسَّاعَةُ وَهُمْ أَحْيَاءٌ، وَاَلَّذِينَ يَتَّخِذُونَ الْقُبُورَ مَسَاجِدَ)) وَرَوَاهُ أَبُو حَاتِمٍ فِي صَحِيحِهِ
Ahmad kwa isnaad nzuri kutoka kwa Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه) amesimulia Hadiyth Marfuw’: ((Hakika watu waovu kabisa kitakaowadiriki Qiyaamah nao ni hai, na wale wanaofanya makaburi kuwa ni Misikiti [mahali pa ‘ibaadah])) [Ahmad na amesimulia Abuu Haatim katika Swahiyh yake]
Masuala Muhimu Yaliyomo:
1-Onyo la Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu ujenzi wa Misikiti ya kumwabudu Allaah katika makaburi ya watu wema, hata kama anayefanya hivyo ana niyyah njema.
2-Haramisho la masanamu na vitu kama hivyo (mapicha) na uzito wa jambo hilo.
3-Funzo katika msisitizo wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) wakati wa kufikisha hili, ambapo kwanza aliwaeleza (kwa upole), kisha siku tano kabla hajafariki alisema kama hapo awali. Halafu baadaye wakati wa Sakaraatul-Mawti akarudia hilo hilo.
4-Aliharamisha kwa kusisitiza kuwa hili lisifanywe kaburini kwake, kabla ya kuweko kaburi lenyewe.
5-Hiyo ni miongoni mwa matendo ya Wayahudi na Wakristo kuhusu makaburi ya Manabii wao.
6-Aliwalaani Mayahudi na Wakristo kwa sababu hiyo.
7-Kusudio la kufanya hivyo ni kutuonya sisi kuhusu kaburi lake tusilifanyie ‘ibaadah.
8-Sababu ya kutokujengewa kaburi lake.
9-Maana halisi ya: (makaburi) “kuyafanya Misikiti.”
10-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amefananisha wanaofanya makaburi kuwa Misikiti na watakaodiriki Qiyaamah wakiwa hai. Akataja njia zinazopeleka katika shirki kabla hazijatokea, pamoja na natija zake.
11-Alilitaja hili siku tano kabla hajafariki. Hapa kuna kukanusha makundi mawili ambao ni miongoni mwa waovu zaidi katika watu wa bid’ah (uzushi). Bali baadhi ya Wanachuoni wameyatenga kabisa makundi hayo mawil kutoka ule mjumuiko wa makundi 72 ya Waislamu. Mawili hayo ni Ar-Raafhidhwah (Shia) na Aj-Jahmiyyah. Na ni kwa sababu ya Raafidhwah ndio ikaanza shirki ya kufanya ‘ibaadah ya makaburi nao ndio wa kwanza kuyajengea Misikiti.
12-Kuteseka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Sakaartul-Mawt.
13-Allaah (سبحانه وتعالى) Amemkirimu kumfanya kuwa ni khalili.
14-Ubainisho kuwa ukhalili huo ulikuwa zaidi ya upendo mwingine.
15-Ubainisho kuwa Abuu Bakr Asw-Swiddiyq (رضي الله عنه) ni Swahaba alikuwa ni mbora wa Maswahaba.
16-Ishara ya ukhalifa wa (Abuu Bakr).