25-Kitaab At-Tawhiyd: Bainisho La Aina Za Uchawi

Mlango Wa 25

بَابُ بَيَانِ شَيْءٍ مِنْ أَنْوَاعِ السِّحْرِ

Bainisho La Aina Za Uchawi


 

 

قَالَ أَحْمَدُ حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ جَعْفَرٍ، حَدَّثَنَا عَوْفٌ عَنْ حَيَّانَ بْنِ الْعَلاءِ،  حَدَّثَنَا قَطَنُ بْنُ قَبِيصَةَ عَنْ أَبِيهِ أَنَّهُ سَمِعَ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((إِنَّ الْعِيَافَةَ وَالطَّرْقَ وَالطِّيَرَةَ مِنَ الْجِبْتِ))

Imaam Ahmad amesema: Muhammad bin Ja’far amesimulia kutoka kwa ‘Awf, kutoka kwa Hayyaan bin Al-‘Alaa, kutoka kwa Qatwanu bin Qabiyswah, kutoka kwa baba yake kwamba kamsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Hakika Al-’Iyaafah na Atw-Twarqa na Atw-Twiyaarah ni Al-Jibt [uchawi])) [Ahmad]

 

قَالَ عَوْفٌ الْعِيَافَةُ زَجْرُ الطَّيْرِ، وَالطَّرْقُ الْخَطُّ يُخَطُّ بِالأَرْضِ

Amesema Al-‘Awf:

Al-’Iyaafah :           ni kumwacha ndege aruke itabiriwe jambo.

Atw-Twarqa:         ni kuchora mistari ardhini [kutabiri jambo]. 

Atw-Twiyaarah:  Itikadi za ushirikina kutumia ndege kuruka ili kubashiria ya ghayb; mkosi, nuksi).

 

وَالْجِبْتُ قَالَ الْحَسَنُ رَنَّةُ الشَّيْطَانِ إِسْنَادُهُ جَيِّدٌ

Na Hasan Al-Baswri amesema Al-Jibt ni kusikiliza sauti ya shaytwaan [Isnaad yake ni nzuri]

 

وَلأَبِي دَاوُدَ وَالنَّسَائِيِّ وَابْنِ حِبَّانَ فِي صَحِيحِهِ لَهُمُ الْمُسْنَدُ مِنْهُ

Na Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy na Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake wana isnaad nzuri ya Hadiyth hiyo.

 

 وَعَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((مَنِ اِقْتَبَسَ شُعْبَةً مِنَ النُّجُومِ، فَقَدِ اِقْتَبَسَ شُعْبَةً مِنَ السِّحْرِ، زَادَ مَا زَادَ)) رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ وَإِسْنَادُهُ صَحِيحٌ

Na Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Atakayesomea unajimu [utabiri wa nyota] basi amefanya uchawi, kadiri anavyozidisha ndivyo kosa lake linavyozidi [madhambi])) [Abuu Daawuwd na isnaad yake Swahiyh]

 

وَلِلنَّسَائِيِّ مِنْ حَدِيثِ أَبِي هُرَيْرَة: ((مَنْ عَقَدَ عُقْدَةً ثُمَّ نَفَثَ فِيهَا فَقَدْ سَحَرَ، وَمَن ْسَحَرَ فَقَدْ أَشْرَكَ، وَمَنْ تَعَلَّقَ شَيْئًا وُكِلَ إِلَيْهِ))

Na An-Nasaaiy kutoka Hadiyth ya Abu Hurayrah: ((Atakayefunga fundo kisha akalipuliza amefanya uchawi. Na atakayefanya uchawi amefanya shirki, na atakayetundika kitu [talasimu, au kuvaa hirizi, zindiko] basi amejiweka katika ulinzi wa hicho kitu alichokivaa)) [na itamdhalilisha]))

 

وَعَنِ اِبْنِ مَسْعُودٍ (رضي الله عنه) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((أَلاَ هَلْ أُنَبِّئُكُمْ مَا الْعَضْهُ؟ هِيَ النَّمِيمَةُ، الْقَالَةُ بَيْنَ النَّاسِ))  رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Na Imepokelewa kutoka kwa Ibn Mas’uwd(رضي الله عنه)  kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Je, nikujulisheni nini Al-’Adhw-hu? Ni An-Namiymah kwa ajili ya kueneza uovu kati ya watu)) [An-Nasaaiy]

 

Al-’Adhw-hu:  kueneza uongo, uchawi n.k.

 

An-Namiymah: kupeleka uvumi kwa ajili ya kufitinisha na kugombanisha watu.

 

وَلَهُمَا عَنِ اِبْنِ عُمَرَ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((إِنَّ مِنَ الْبَيَانِ لَسِحْرًا))

Nao wawili [Al-Bukhaariy na Muslim] kutoka kwa Ibn ‘Umar  (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا)  kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Hakika katika ufasaha mwengine kuna uchawi)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Al-‘Iyaafah, At-Twarqa na At-Twiyaarah ni aina tatu za uchawi.

 

2-Al-‘Iyaafah na At-Twarqa zimeelezewa.

 

3- Unajimu pia ni namna ya uchawi.

 

4-Kufunga vifundo na kuvipulizia pia ni uchawi.

 

5-An-Namiymah nayo ni namna ya uchawi.

 

6-Wakati mwengine kuzungumza kwa ufasaha hadi ukazidi mno nao ni uchawi.

 

 

 

 

Share