26-Kitaab At-Tawhiyd: Kuhusu Makuhani Na Mfano Wao

Mlango Wa 26

بَابُ مَا جَاءَ فِي الْكُهَّانِ وَنَحْوِهِمْ

Kuhusu Makuhani Na Mfano Wao


 

 

رَوَى مُسْلِمٌ فِي صَحِيحِهِ عَنْ بَعْضِ أَزْوَاجِ النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) عَنِ النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((مَنْ أَتَى عَرَّافًا فَسَأَلَهُ عَنْ شَيْءٍ فَصَدَّقَهُ، لَمْ تُقْبَلْ لَهُ صَلاةٌ أَرْبَعِينَ يَوْمًا))

Amesimulia Muslim katika Swahiyh yake kutoka baadhi ya wake wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Atakayemwendea mtabiri akamuuliza kitu kisha akamuamini, haitokubaliwa Swalaah yake siku arubaini)) [Muslim]

 

 وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) عَنِ النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)  قَالَ: ((مَنْ أَتَى كَاهِنًا، فَصَدَّقَهُ بِمَا يَقُولُ فَقَدْ كَفَرَ بِمَا أُنْزِلَ عَلَى مُحَمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)) رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Atakayemkaribia kuhani na kuamini anayoyasema basi amekanusha aliyoteremshiwa Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)) [Abuu Daawuwd]

 

وَلِلأَرْبَعَةِ وَالْحَاكِمِ وَقَالَ:صَحِيحٌ عَلَى شَرْطِهِمَا  عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ: ((مَنْ أَتَى عَرَّافًا أَوْ كَاهِنًا فَصَدَّقَهُ بِمَا يَقُولُ فَقَدْ كَفَرَ بِمَا أُنْزِلَ عَلَى مُحَمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ))

Na wasimuliaji wengine wanne wa Hadiyth na Al-Haakim wamenakilii Hadiyth ya Abuu Hurayrah(رضي الله عنه)  na wameikiri ni Swahiyh kwa mujibu wa masharti yao kwamba: ((Atakayemwendea mtabiri au kuhani akamwamini ayasemayo basi amekanusha aliyoteremshiwa Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم )) 

 

وَلأَبِي يَعَلَى بِسَنَدٍ جَيِّدٍ عَنِ ابْنِ مَسْعُودٍ مِثْلُهُ مَوْقُوفًا

Na Abuu Ya’laa ameripoti Hadiyth kama hiyo kutoka kwa Ibn Mas’uwd kwa isnaad nzuri lakini ni Hadiyth Mawquwf.  

 

وَعَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَينٍ مَرْفُوعًا: ((لَيْسَ مِنَّا مَنْ تَطَيَّرَ أَوْ تُطُيِّرَ لَهُ، أَوْ تَكَهَّنَ أَوْ تُكُهِّنَ لَهُ، أَوْ سَحَرَ أَوْ سُحِرَ لَهُ، وَمَنْ أَتَى كَاهِنًا فَصَدَّقَهُ بِمَا يَقُولُ، فَقَدْ كَفَرَ بِمَا أُنْزِلَ عَلَى مُحَمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)) رَوَاهُ الْبَزَّارُ بِإِسْنَادٍ جَيِّدٍ

Na Imepokelewa toka kwa ‘Imraan bin Huswayn Hadiyth Marfuw’: ((Si miongoni mwetu anayetafuta au anayebashiriwa Atw-Twiyaarah (mkosi, nuksi) au akafanya ukuhani au akafanyiwa ukuhani, au anayefanya uchawi au anayefanyiwa uchawi, na atakayemwendea kuhani akamwamini ayasemayo basi amekanusha aliyoteremshiwa Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)) [Al-Bazaar kwa isnaad nzuri]

 

وَرَوَاهُ الطَّبَرَانِيُّ فِي الْأَوْسَطِ بِإِسْنَادٍ حَسَنٍ مِنْ حَدِيثِ ابْنِ عَبَّاسٍ دُونَ قَوْلِهِ: ((وَمَنْ أَتَى)) .. إِلَى آخِرِهِ

Hadiyth hiyo hiyo ameinakili Atw-Twabaraaniy katika Al-Awsatw kwa isnaad nzuri kutoka kwa Ibn ‘Abbaas bila ya kauli ya mwisho: ((Na atakayemwendea…)) 

 

قَالَ الْبَغَوِيُّ :الْعَرَّافُ الَّذِي يَدَّعِي مَعْرِفَةَ الأُمُورِ بِمُقَدِّمَاتٍ يُسْتَدَلُّ بِهَا عَلَى الْمَسْرُوقِ وَمَكَانِ الضَّالَّةِ وَنَحْوِ ذَلِكَ

Al-Baghaawiy amesema: Al-‘Arraaf (mtabiri) ni ambaye anadai ujuzi wa mambo fulani kama vile yanayohusu vitu vilivyoibiwa, wapi vipo vitu hivyo, au mnyama aliyepotea na kama hayo kwa njia ya uchawi.

وَقِيلَ هُوَ الْكَاهِنُ، وَالْكَاهِنُ هُوَ الَّذِي يُخْبِرُ عَنِ الْمُغَيَّبَاتِ فِي الْمُسْتَقْبَلِ

Wengine wamesema yeye ndiye kuhani, na kuhani ni anayetoa khabari za mustaqbal (za mbele) zilizofichikana.

 

وَقِيلَ الَّذِي يُخْبِرُ عَمَّا فِي الضَّمِيرِ

Na wengine wamesema ni ambaye anayetoa yaliyo katika dhamira ya mtu (siri moyoni).

 

وَقَالَ أَبُو الْعَبَّاسِ ابْنُ تَيْمِيَّةَ الْعَرَّافُ اسْمٌ لِلْكَاهِنِ، وَالْمُنَجِّمِ وَالرَّمَّالِ وَنَحْوِهِمْ مِمَّنْ يَتَكَلَّمُ فِي مَعْرِفَةِ الأُمُورِ بِهَذِهِ الطُّرُقِ

Na Abul-‘Abbaas, Ibn Taymiyyah kasema: Al-‘Arraaf ni jina la kuhani, na Al-Munajjim (mtabiri wa nyota) na Ar-Rammaal (mpiga ramli) na kama hao wanaojidai kuyajua mambo kwa njia hizo.

 

 وَقَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ فِي قَوْمٍ يَكْتُبُونَ: أَبَا جَادٍ. وَيَنْظُرُونَ فِي النُّجُومِ مَا أَرَى مَنْ فَعَلَ ذَلِكَ لَهُ عِنْدَ اللَّهِ مِنْ خَلاقٍ

Na Ibn ‘Abbaas akasema kuhusu watu wanaoandika ‘Abaa-Jaad’ (alfabeti kutumilia utabiri, uaguzi) na wanatazamia nyota kuamini athari zake ardhini. “Sioni kuwa wana fungu lolote mbele ya Allaah.”

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Kumwamini kuhani na kuamini Qur-aan ni iymaan ambazo haziwezi kuwa pamoja katika moyo wa mtu mmoja.

 

2-Tangazo kuwa kufanya hivyo (kumwamini kuhani) ni kufuru.

 

3-Kutajwa mtu anayetabiriwa.

 

4-Kutajwa aliyefanyiwa itikadi za ushirikina.

 

5-Kutajwa aliyefanyiwa uchawi.

 

6-Kutajwa anayejifundisha Abaa-Jaad (kutumia alfabeti katika utabiri, uaguzi)  

 

7-Tofauti baina ya kuhani na mtabiri.

 

 

 

Share