27-Kitaab At-Tawhiyd: An-Nushrah: Kuagua Uchawi Kwa Uchawi
Mlango Wa 27
بَابُ مَا جَاءَ فِي النُّشْرَةِ
An-Nushrah: Kuagua Uchawi Kwa Uchawi
عَنْ جَابِر: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) سُئِلَ عَنْ النُّشْرَةِ فَقَالَ: ((هِيَ مِنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ)) رَوَاهُ أَحْمَدُ بِسَنَدٍ جَيِّدٍ وَأَبُو دَاوُدَ وَقَالَ: سُئِلَ أَحْمَدُ عَنْهَا: فَقَالَ ابْنُ مَسْعُودٍ يَكْرَهُ هَذَا كُلَّهُ
Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliulizwa kuhusu An-Nushrah akasema: ((Hicho ni kitendo cha shaytwaan)) [Ahmad kwa isnaad nzuri na Abuu Daawuwd]
Na Abuu Daawuwd akasema: Aliulizwa Imaam Ahmad kuhusu hiyo [An-Nushrah] akasema: Ibn Mas’uwd alikuwa akichukizwa na yote hayo.
وَفِي "الْبُخَارِيِّ: عَنْ قَتَادَةَ: قُلْتُ لابْنِ الْمُسَيِّبِ: رَجُلٌ بِهِ طِبٌّ أَوْ يُؤْخَذُ عَنِ امْرَأَتِهِ، أَيُحَلُّ عَنْهُ أَوْ يُنْشَرُ؟ قَالَ: لاَ بَأْسَ بِهِ إِنَّمَا يُرِيدُونَ بِهِ الإِصْلاحَ، فَأَمَّا مَا يَنْفَعُ فَلَمْ يُنْهَ عَنْهُ
Na katika Al-Bukhaariy amesimulia kutoka kwa Qataadah(رضي الله عنه) : “Nilimuuliza Ibn Al-Musayyib: Mtu akiwa karogwa au ambaye hawezi unyumba (kumuingilia mkewe), je, ni sawa kuaguliwa kwa uchawi au tutumie njia nyingine za matibabu?” Ibn Al-Musayyib akajibu: Hapana ubaya kwa sababu wanakusudia kutengeneza. Yanayonufaisha [na kuondosha madhara] hayakukatazwa.
وَرُوِيَ عَنِ الْحَسَنِ أَنَّهُ قَالَ: لا يَحِلُّ السِّحَرَ إِلاَّ سَاحِرٌ.
Na imesimuliwa kutoka kwa Hasan Al-Baswriy kwamba amesema: Mchawi pekee anaweza kuagua uchawi wa mchawi mwengine”
قال ابْنُ الْقَيِّمِ: النُّشْرَةُ حَلُّ السِّحَرِ عَنِ الْمَسْحُورِ، وَهِيَ نَوْعَانِ:
Ibn Al-Qayyim amesema: An-Nushrah ni kuondosha uchawi wa aliyerogwa. Nazo ni aina mbili:
أَحَدُهُمَا حَلٌّ بِسِحْرٍ مِثْلِهِ، وَهُوَ الَّذِي مِنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ وَعَلَيْهِ يُحْمَلُ قَوْلُ الْحَسَنِ، فَيَتَقَرَّبُ النَّاشِرُ وَالْمُنْتَشَرُ إِلَى الشَّيْطَانِ بِمَا يُحِبُّ فَيُبْطِلُ عَمَلَهُ عَنِ الْمَسْحُورِ
Ya kwanza: Kuondosha uchawi kwa kutumia uchawi mwengine; na hicho ni kitendo cha shaytwaan (nayo ni haraam). Na hayo ndio maelezo ya Hasan kwamba mchawi na aliyerogwa, wote wanamkaribia shaytwaan kwa ayapendayo. Kisha shaytwaan humuondeshea aliyerogwa athari za uchawi.
وَالثَّانِي النُّشْرَةُ بِالرُّقْيَةِ وَالتَّعَوُّذَاتِ وَالأَدْوِيَةِ وَالدَّعَوَاتِ الْمُبَاحَةِ، فَهَذَا جَائِزٌ
Ya pili: Ni kutibu uchawi kwa Ruqyah (Aayah za Qur-aan na adhkaar za Sunnah), dawa na du´aa zinazokubalika; hii inajuzu.
Masuala Muhimu Yaliyomo:
1-Kukatazwa An-Nushrah.
2-Tofauti kati ya aina ya An-Nushrah inayojuzu na iliyoharamishwa katika kuondosha matatizo hayo.