32-Kitaab At-Tawhiyd: Kumkhofu Allaah Pekee Katika Yanayomhusu Yeye Ta’aalaa
Mlango Wa 32
باب: إِنَّمَا ذَٰلِكُمُ الشَّيْطَانُ يُخَوِّفُ أَوْلِيَاءَهُ...
Kumkhofu Allaah Pekee Katika Yanayomhusu Yeye Ta’aalaa
قَوْلِ اللَّهِ تَعَالَى :
Kauli ya Allaah Ta’aalaa:
إِنَّمَا ذَٰلِكُمُ الشَّيْطَانُ يُخَوِّفُ أَوْلِيَاءَهُ
((Hakika huyo ni shaytwaan anawakhofisha marafiki wake wandani)) [Aal-‘Imraan (3: 175)]
وَقَوْلِهِ:
Na kauli Yake:
إِنَّمَا يَعْمُرُ مَسَاجِدَ اللَّـهِ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَأَقَامَ الصَّلَاةَ وَآتَى الزَّكَاةَ وَلَمْ يَخْشَ إِلَّا اللَّـهَ ۖ فَعَسَىٰ أُولَـٰئِكَ أَن يَكُونُوا مِنَ الْمُهْتَدِينَ ﴿١٨﴾
((Hakika wanaoamirisha Misikiti ya Allaah ni (wale) wanaomwamini Allaah na Siku ya Mwisho, na wakasimamisha Swalaah na wakatoa Zakaah na hawamkhofu (yeyote) isipokuwa Allaah. Basi asaa hao wakawa miongoni mwa walioongoka)) [At-Tawbah (9: 18)]
وَقَوْلِهِ:
Na kauli Yake:
وَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ آمَنَّا بِاللَّـهِ فَإِذَا أُوذِيَ فِي اللَّـهِ جَعَلَ فِتْنَةَ النَّاسِ كَعَذَابِ اللَّـهِ وَلَئِن جَاءَ نَصْرٌ مِّن رَّبِّكَ لَيَقُولُنَّ إِنَّا كُنَّا مَعَكُمْ ۚ أَوَلَيْسَ اللَّـهُ بِأَعْلَمَ بِمَا فِي صُدُورِ الْعَالَمِينَ ﴿١٠﴾
((Na miongoni mwa watu wako wasemao: “Tumemwamini Allaah;” lakini wanapoudhiwa kwa ajili ya Allaah, hufanya fitnah za watu kama kwamba ni adhabu ya Allaah. Na inapowajia nusura kutoka kwa Rabb wako husema: “Hakika sisi tulikuwa pamoja nanyi.” Je, kwani Allaah Hayajui yale yaliyomo katika vifua vya walimwengu?)) [Al-‘Ankabuwt (29: 10)]
عَنْ أَبِي سَعِيدٍ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) مَرْفُوعًا: ((إِنَّ مِنْ ضَعْفِ الْيَقِينِ أَنْ تُرْضِيَ النَّاسَ بِسَخَطِ اللَّهِ، وَأَنْ تَحْمَدَهُمْ عَلَى رِزْقِ اللَّهِ، وَأَنْ تَذُمَّهُمْ عَلَى مَا لَمْ يُؤْتِكَ اللَّهُ، إِنَّ رِزْقَ اللَّهِ لا يَجُرُّهُ حِرْصُ حَرِيصٍ، وَلا يَرُدُّهُ كَرَاهِيَةُ كَارِه))
Abuu Sa’iyd(رضي الله عنه) amesimulia Hadiyth Marfuw’: ((Hakika katika udhaifu wa yakini ni kuridhisha wengine hali ya kumuudhi Allaah, na kuwasifu [na kuwashukuru] wengine kwa rizki Aliyotoa Allaah, na kuwalaumu wengine kwa asilokujaalia Allaah. Hakika rizki ya Allaah haivutwi na bidii au pupa ya wenye pupa, wala haizuiwi na chuki ya mwenye inda)) [Abuu Nu’aym, Al-Hilyah]
وَعَنْ عَائِشَةَ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((مَنِ الْتَمَسَ رِضَا اللَّهِ بِسَخَطِ النَّاسِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ وَأَرْضَى عَنْهُ النَّاسَ، وَمَنِ الْتَمَسَ رِضا النَّاسِ بِسَخَطِ اللَّهِ سَخِطَ اللَّهُ عَلَيْهِ وَأَسْخَطَ عَلَيْهِ النَّاسَ)) رَوَاهُ ابْنُ حِبَّانَ فِي صَحِيحِهِ
Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Atakayemridhisha Allaah hata ikiwa watu watakasirika, huyo atapata radhi za Allaah pamoja na radhi za watu, kwa vile Allaah Atawafanya watu wamridhiye yeye. Na atakayewaridhisha watu hali ya kumkasirisha Allaah, huyo atakasirikiwa na Allaah pamoja na watu kwa vile Allaah Atawafanya watu wamkasirikie)) [Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake]
Masuala Muhimu Yaliyomo:
1-Tafsiri ya Aayah katika Suwrah Aal-‘Imraan (3: 175).
2-Tafsiri ya Aayah katika Suwrah At-Tawbah (9: 18).
3-Tafsiri ya Aayah katika Suwrah Al-‘Ankabuwt (29: 10).
4-Kuna mabadiliko ya kupanda na kushuka iymaan, huwa dhaifu na wakati mwengine huwa ni ya juu kabisa.
5-Dalili tatu za udhaifu wa yakini na iymaan ya mtu.
6-Kumpwekesha Allaah (سبحانه وتعالى) Pekee kwa kumkhofu ni wajibu (katika Uislamu).
7-Malipo ya mtu anayemkhofu Allaah (سبحانه وتعالى) Pekee kwa ikhlaasw kabisa.
8-Adhabu ya asiyemkhofu Allaah (سبحانه وتعالى).