33-Kitaab At-Tawhiyd: Kutawakali Kwa Allaah Pekee

Mlango Wa 33

باب:  وَعَلَى اللَّـهِ فَتَوَكَّلُوا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ

Kutawakali Kwa Allaah Pekee


بَابُ قَوْلِ اَللَّهِ تَعَالَى:

Mlango kuhusu kauli ya Allaah Ta’aalaa:

 

  وَعَلَى اللَّـهِ فَتَوَكَّلُوا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٢٣﴾

((Na kwa Allaah Pekee tawakalini ikiwa nyinyi ni Waumini)) [Al-Maaidah (5: 23)]

وَقَوْلِهِ:

Na kauli Yake:

 

 إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّـهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ آيَاتُهُ زَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ ﴿٢﴾

((Hakika Waumini ni wale ambao Anapokumbukwa na kutajwa Allaah, nyoyo zao zinajaa khofu na wanaposomewa Aayaat Zake huwazidishia iymaan, na kwa Rabb wao wanatawakali)) [Al-Anfaal (8: 2)]

 وَقَوْلِهِ:

Na kauli Yake:

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ حَسْبُكَ اللَّـهُ وَمَنِ اتَّبَعَكَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٦٤﴾

((Ee Nabiy! Anakutosheleza Allaah na anayekufuata miongoni wa Waumini)) [Al-Anfaal (8: 64)]

 وَقَوْلِهِ:

Na kauli Yake:

  وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ فَهُوَ حَسْبُهُ ۚ  

((Na yeyote anayetawakali kwa Allaah, basi Yeye Humtosheleza)) [Atw-Twalaaq (65: 3)]

 

 وَعَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ قَالَ: حَسْبُنَا اَللَّهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ، قَالَهَا إِبْرَاهِيمُ عَلَيْهِ اَلسَّلامُ حِينَ أُلْقِيَ فِي اَلنَّارِ، وَقَالَهَا مُحَمَّدٌ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) حِينَ قَالُوا لَهُ: ((الَّذِينَ قَالَ لَهُمُ النَّاسُ إِنَّ النَّاسَ قَدْ جَمَعُوا لَكُمْ فَاخْشَوْهُمْ فَزَادَهُمْ إِيمَانًا وَقَالُوا حَسْبُنَا اللَّـهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ ﴿١٧٣﴾ رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ وَالنَّسَائِيُّ

Na Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  amesema: ‘Hasbuna-Allaahu wa Ni’mal-Wakiyl Amesema hivyo Ibraahiym alipotupwa motoni. Na amesema hivyo Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) waliposema: ((Wale walioambiwa na watu: “Hakika watu wamejumuika dhidi yenu, basi waogopeni” Lakini iliwawazidishia iymaan wakasema: “Hasbuna-Allaah! Allaah Anatutosheleza, Mzuri Alioje Mdhamini Anayetegemewa kwa yote)) [Aal-‘Imraan (2: 173)]

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Kuwa na tawakkul kwa Allaah (سبحانه وتعالى) ni wajibu wa Dini.

 

2-Kuwa na tawakkul kwa Allaah (سبحانه وتعالى) ni sharti la iymaan.

 

3-Tafsiri ya Aayah katika Suwrah Al-Anfaal (8: 2).

 

4-Tafsiri ya Aayah katika Suwrah Al-Anfaal (8: 64).

 

5-Tafsiri ya Aayah katika Suwrah Atw-Twalaaq (65: 3).

 

6-Umuhimu wa maneno: ((Hasbuna-Allaahu wa Ni’mal-Wakiyl - Haya ni maneno yaliyosemwa na Ibraahiym (عليه السلام)   na Nabiy Muhammad   (صلى الله عليه وآله وسلم) wakati wa janga.

Share