44-Kitaab At-Tawhiyd: Msemo: “Kwa Kupenda Allaah Na Kupenda Kwako”

Mlango Wa 44

بَابٌ: قَوْلُ مَا شَاءَ اللَّهُ وَشِئْتَ

Msemo: “Kwa Kupenda Allaah Na Kupenda Kwako


 

 

عَنْ قُتَيْلَةَ: أَنَّ يَهُودِيًّا أَتَى النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فَقَالَ: إِنَّكُمْ تُشْرِكُونَ، تَقُولُونَ مَا شَاءَ اللَّهُ وَشِئْتَ، وَتَقُولُونَ وَالْكَعْبَةِ فَأَمَرَهُمُ النَّبِيُّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) إِذَا أَرَادُوا أَنْ يَحْلِفُوا أَنْ يَقُولُوا: وَرَبِّ الْكَعْبَةِ وَأَنْ يَقُولُوا: مَا شَاءَ اللَّهُ ثُمَّ شِئْتَ.  رَوَاهُ النَّسَائِيُّ وَصَحَّحَهُ

Imepokelewa kutoka kwa Qutaylah (رضي الله عنه) kwamba: Myahudi alimwendea Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: Nyinyi mnafanya shirki pindi mnaposema: “Kwa kupenda Allaah na kupenda kwako (ee Muhammad”, na mnasema: “Naapa kwa Al-Ka’bah.” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akawaamrisha Maswahaba kuwa wakitaka kuapa waseme: ((“Naapa kwa Rabb Wa Al-Ka’bah” na waseme: “Kwa kupenda Allaah na kisha kwa kupenda kwako [ee Muhammad]”)) [An-Nasaaiy na ameikiri Swahiyh]

 

وَلَهُ أَيْضًا عَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ: أَنَّ رَجُلاً قَالَ لِلنَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: مَا شَاءَ اللَّهُ وَشِئْتَ، فَقَالَ: ((أَجَعَلْتَنِي لِلَّهِ نِدًّا؟ بَلْ! مَا شَاءَ اللَّهُ وَحْدَهُ))

(An-Nasaaiy) amesimulia pia kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) : Mtu mmoja alimwambia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): “Kwa kupenda Allaah na kupenda kwako”, Akamjibu: ((Je, umenilinganisha na Allaah? Bali sema: Kwa kupenda Allaah Peke Yake”))

 

وَلابْنِ مَاجَهْ: عَنِ الطُّفَيْلِ أَخِي عَائِشَةَ لأُمِّهَا، قَالَ: رَأَيْتُ كَأَنِّي أَتَيْتُ عَلَى نَفَرٍ مِنَ الْيَهُودِ،  قُلْتُ:  إِنَّكُمْ لأَنْتُمُ الْقَوْمُ، لَوْلا أَنَّكُمْ تَقُولُونَ: عُزَيْرٌ ابْنُ اللَّهِ.  قَالُوا: وَأَنْتُمْ لأَنْتُمُ الْقَوْمُ، لَوْلا أَنَّكُمْ تَقُولُونَ: مَا شَاءَ اللَّهُ وَشَاءَ مُحَمَّدٌ. ثُمَّ مَرَرْتُ بِنَفَرٍ مِنْ النَّصَارَى فَقُلْتُ: إِنَّكُمْ لأَنْتُمُ الْقَوْمُ، لَوْلا أَنَّكُمْ تَقُولُونَ: الْمَسِيحُ ابْنُ اللَّهِ. قَالُوا: وَإِنَّكُمْ لأَنْتُمُ الْقَوْمُ، لَوْلا أَنَّكُمْ تَقُولُونَ: مَا شَاءَ اللَّهُ وَشَاءَ مُحَمَّدٌ.  فَلَمَّا أَصْبَحْتُ أَخْبَرْتُ بِهَا مَنْ أَخْبَرْتُ، ثُمَّ أَتَيْتُ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فَأَخْبَرْتُهُ، فَقَالَ: ((هَلْ أَخْبَرْتَ بِهَا أَحَدًا؟)) قُلْتُ: نَعَمْ . قَالَ: فَحَمِدَ اللَّهَ وَأَثْنَى عَلَيْهِ ثُمَّ قَالَ: ((أَمَّا بَعْدُ؛ فَإِنَّ طُفَيْلاً رَأَى رُؤْيَا أَخْبَرَ بِهَا مَنْ أَخْبَرَ مِنْكُمْ، وَأَنَّكُمْ قُلْتُمْ كَلِمَةً يَمْنَعُنِي كَذَا وَكَذَا أَنْ أَنْهَاكُمْ عَنْهَا فَلا تَقُولُوا: مَا شَاءَ اللَّهُ وَشَاءَ مُحَمَّدٌ، وَلَكِنْ قُولُوا مَا شَاءَ اللَّهُ وَحْدَهُ))

Na Ibn Maajah amesimulia kutoka kwa Twufayl ambaye ni kaka yake ‘Aaishah kwa mama, kwamba amesema: “Niliota katika utoto kuwa nilikutana na kundi la Mayahudi nikawaambia: Mngelikuwa nyinyi ndio waja wema wa Allaah lau si kusema kwenu kuwa ‘Uzayr ni mwana wa Allaah.” Wakasema: “Mngekuwa nyinyi (Waislamu) ndio waja wema wa Allaah lau si kusema kwenu: “Kwa kupenda Allaah na kupenda Muhammad.” Kisha nikakutana na kundi la Wakristo nikawaambia: “Mngekuwa nyinyi ndio waja wema wa Allaah lau si kusema kwenu kuwa Masiyhi ni mwana wa Allaah.” Wakasema: “Mngekuwa nyinyi Waislamu ndio waja wema wa Allaah lau si kusema kwenu: “Kwa kupenda Allaah na kupenda Muhammad.” Nilipoamka nikawahadithia ndoto yangu niliowahadithia kisha nikamwendea Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) nikamuhadithia. Akaniuliza: ((Je, umemhadithia yeyote?)) Nikasema: “Ndio.” Akapanda juu ya mimbari Akamhimidi Allaah (سبحانه وتعالى) na kumtukuza, kisha akasema: ((Amma ba’ad: Hakika Twufayl ameota ndoto na ameshawahi kuwahadithia aliowahi kuwahadithia miongoni mwenu. Na hakika mlikuwa mkisema msemo ambao sikuwazuia kwa sababu kadhaa wa kadhaa. Hivyo msiseme: “Kwa kupenda Allaah na kupenda Muhammad”, bali semeni: “Kwa kupenda Allaah Pekee Yake”)) [Ibn Maajah]

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Mayahudi walikuwa wakitambua shirki ndogo.

 

2-Fahamu ya mtu kuhusu shirki ikiwa atapenda kutenda. 

 

3-Kauli ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): ((Je, umenilinganisha na Allaah?)) Imelaumiwa kwa kiasi kikubwa basi ubaya ulioje wa mshairi aliyesema:

 يا أكرمَ الخلْقِ مَالِىْ مَنْ اَلُوْذُ بِه سِوَاك عند حدوثِ الحادثِ العَمم    

“Ee mbora wa viumbe, sina mwengine kumuomba kinga isipokuwa wewe wakati wa dhiki na misukosuko.”[1] (Na beti zinazofuatia).

 

4-Hii si shirki kubwa kwa vile Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alivyosema:  

((Sikuwazuia kwa sababu kadhaa wa kadhaa)).

 

5-Ndoto ya kweli ni aina ya Wahyi.

 

6-Ndoto ya maana na ya kweli inaweza kuwa sababu ya kuanzisha hukumu fulani katika Shariy'ah.

 

 

 

 

 

[1] Shairi la Burdah la Al-Buswayriy ambalo beti zake zinamshirikisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kumpa cheo kama cha Allaah (سبحانه وتعالى).

Share