45-Kitaab At-Tawhiyd: Anayetukana Wakati Amemuudhi Allaah

Mlango Wa 45

بَابٌ مَنْ سَبَّ الدَّهْرَ فَقَدْ آذَى اللَّهَ

Anayetukana Wakati Amemuudhi Allaah


 

 

وَقَوْلُ اَللَّهِ تَعَالَى:

Na kauli ya Allaah Ta’aalaa:

 

وَقَالُوا مَا هِيَ إِلَّا حَيَاتُنَا الدُّنْيَا نَمُوتُ وَنَحْيَا وَمَا يُهْلِكُنَا إِلَّا الدَّهْرُ ۚ وَمَا لَهُم بِذَٰلِكَ مِنْ عِلْمٍ ۖ إِنْ هُمْ إِلَّا يَظُنُّونَ ﴿٢٤﴾

((Na wakasema: “Huu si chochote isipokuwa ni uhai wetu wa dunia, tunakufa na tunahuika, na hakuna cha kutuangamiza isipokuwa zama tu.” Na wala hawana kwayo ujuzi wowote, ila wao wanadhania tu)) [Al-Jaathiyah (45: 24)]

 

وَفِي الصَّحِيحِ: عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنِ النَّبِيِّ (صَلَى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((قَالَ اللَّهُ تَعَالَى: يُؤْذِينِي ابْنُ آدَمَ يَسُبُّ الدَّهْرَ، وَأَنَا الدَّهْرُ أُقَلِّبُ الْلَّيْلَ وَالنَّهَارَ))

Na katika Swahiyh, Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Allaah Ta’aalaa Amesema: Bin Aadam ananiudhi, kwani anatukana dahari [wakati au zama], na hali Mimi ni Ad-Dahr [Namiliki kila kitu na uwezo], Nageuza usiku na mchana)).

 

وَفِي رِوَايَةٍ: ((لا تَسُبُّوا الدَّهْرَ؛ فِإنَّ اللَّهَ هُوَ الدَّهْرُ))

Na katika riwaayah: ((Msitukane dahari kwani hakika Allaah ni Ad-Dahr)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Kulaani wakati kumekatazwa.

 

2-Kutukana wakati ni kumkosoa Allaah (سبحانه وتعالى).

 

3-Kutafakari kauli ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): ((Hakika Allaah ni Ad-Dahr)).

 

4-Jambo linaweza kuwa tusi hata kama haliko katika hisia (za mtukanaji).

 

 

Share