46-Kitaab At-Tawhiyd: Kujiita Qadhi Wa Maqadhi Na Mfano Wake
Mlango Wa 46
بَابٌ التَّسَمِّي بِقَاضِي الْقُضَاةِ وَنَحْوِهِ
Kujiita Qadhi Wa Maqadhi Na Mfano Wake
فِي الصَّحِيحِ: عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنِ النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((إِنَّ أَخْنَعَ اِسْمٍ عِنْدَ اللَّهِ رَجُلٌ تَسَمَّى مَلَكَ الأَمْلاكِ، لاَ مَالِكَ إِلاَّ اللَّهَ))
Katika Swahiyh Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah(رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Jina ovu na la kuchukiza mno kwa Allaah ni mtu kujiita MalakAl-Amlaak [mfalme wa milki zote]. Hakuna Maalik isipokuwa Allaah))
قَالَ سُفْيَانُ مِثْلُ شَاهَانْ شَاهْ .
Sufyaan amesema: mfano: “Shaahaan Shaah” (mfalme wa wafalme kwa Wafursi).
وَفِي رِوَايَةٍ: ((أَغْيَظُ رَجُلٍ عَلَى اللَّهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَأَخْبَثُهُ ))
Na katika riwaayah nyingine:
((Mtu mwenye kuchukiwa mno na muovu kabisa mbele ya Allaah Siku ya Qiyaamah [ni mtu anayejiita: mfalme wa wafalme])) [Al-Bukhaariy]
Na maana ya أخنع ni أوضع: duni, aliyedhalilika kabisa.
Masuala Muhimu Yaliyomo:
1-Kukatazwa kutumia cheo cha ‘mfalme wa wafalme’ kwa yeyote.
2-Kukatazwa mfano wake kama mfano uliotolewa na Sufyaan (رضي الله عنه).
3-Ufahamu na kuelewa uzito wa kauli ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) licha ya kuwa mtu anaweza asidhamirie maana mbaya moyoni mwake.
4-Utambuzi na ufahamu kwamba kutukuzwa kiuabudiwa ni kwa Allaah (سبحانه وتعالى) Pekee Mtukufu kuliko wote, Asiyefikiwa hata chembe ‘Uluwa Yake, Ametakasika na kila kitu (tofauti na ‘mfalme’ wa kidunia).