56-Kitaab At-Tawhiyd: Kisiombwe Chochote Kwa Wajihi Wa Allaah Isipokuwa Jannah
Mlango Wa 56
بَابٌ لا يُسْأَلُ بِوَجْهِ اَللَّهِ إِلاَّ الْجَنَّةُ
Kisiombwe Chochote Kwa Wajihi Wa Allaah Isipokuwa Jannah
عَنْ جَابِرٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((لاَ يُسْأَلُ بِوَجْهِ اَللَّهِ إِلاَّ الْجَنَّةُ)) رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ
Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Kisiombwe chochote kwa Wajihi wa Allaah isipokuwa Jannah)) [Abuu Daawuwd]
Masuala Muhimu Yaliyomo:
1-Makatazo ya kuomba kitu kwa Wajihi wa Allaah (سبحانه وتعالى) isipokuwa Jannah ambayo jambo kuu kabisa.
2-Kuthibitisha Sifa ya Allaah (سبحانه وتعالى) kuwa Ana Wajihi.