57-Kitaab At-Tawhiyd: Kusema: “Lau Isingekuwa Kadhaa Wa Kadhaa”

Mlango Wa 57

بَابٌ مَا جَاءَ فِي الّلو

Kusema: “Lau Isingekuwa Kadhaa Wa Kadhaa”


 

 

وَقَوْلُ اَللَّهِ تَعَالَى:

Na kauli ya Allaah Ta’aalaa:

 

يَقُولُونَ لَوْ كَانَ لَنَا مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ مَّا قُتِلْنَا هَاهُنَا ۗ قُل لَّوْ كُنتُمْ فِي بُيُوتِكُمْ لَبَرَزَ الَّذِينَ كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقَتْلُ إِلَىٰ مَضَاجِعِهِمْ ۖ وَلِيَبْتَلِيَ اللَّـهُ مَا فِي صُدُورِكُمْ وَلِيُمَحِّصَ مَا فِي قُلُوبِكُمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿١٥٤﴾

((Wanasema: “Lau tungelikuwa tuna amri yoyote katika jambo basi tusingeliuliwa hapa.”  Sema: “Lau mngelikuwa majumbani mwenu, bila shaka wangejitokeza wale walioandikiwa kuuwawa kwenye mahali pa kuangukia wafe.” Ili Allaah Ayajaribu yale yaliyomo katika vifua vyenu na Atakase yale yaliyomo katika nyoyo zenu. Na Allaah ni Mjuzi kwa yaliyomo vifuani)) [Aal-‘Imraan (3: 154)]

وَقَوْلُهُ:

Na kauli Yake:

 

الَّذِينَ قَالُوا لِإِخْوَانِهِمْ وَقَعَدُوا لَوْ أَطَاعُونَا مَا قُتِلُوا ۗ قُلْ فَادْرَءُوا عَنْ أَنفُسِكُمُ الْمَوْتَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١٦٨﴾ 

((Wale waliowaambia ndugu zao nao wakakaa (wasiende vitani): “Lau wangelitutii basi wasingeliuawa.” Sema: “Basi ziondoleeni nafsi zenu mauti mkiwa ni wakweli”)) [Aal-‘Imraan (3: 168)]

 

وَفِي اَلصَّحِيحِ عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ) أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((اِحْرِصْ عَلَى مَا يَنْفَعُكَ، وَاسْتَعِنْ بِاَللَّهِ وَلا تَعْجَزَنْ، وَإِنْ أَصَابَكَ شَيْءٌ فَلا تَقُلْ: لَوْ أَنِّي فَعَلْتُ كَذَا لَكَانَ كَذَا وَكَذَا وَلَكِنْ قُلْ: قَدَّرَ اَللَّهُ وَمَا شَاءَ فَعَلَ.  فَإِنَّ (لَوْ) تَفْتَحُ عَمَلَ اَلشَّيْطَانِ))

Na katika Swahiyh [Muslim] Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah(رضي الله عنه)  kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Pupia [kutafuta] yanayokunufaisha na omba msaada kwa Allaah Pekee na usivunjike moyo. Na linapokufika jambo usiseme: ‘Lau kama ningelifanya kadhaa, ingelikuwa kadhaa wa kadhaa’. Bali sema: ‘Qadara-Allaahu wa Maa Shaa Fa’al’ – Amekadiria Allaah na Amefanya Alichotaka - kwani [neno la] ‘lau’ linafungua ‘amali ya shaytwaan)) [Muslim]

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

 

1-Tafsiri ya Aayah mbili Suwrah Aal-'Imraan (3: 154 na 3: 168).

 

2-Kukatazwa waziwazi kusema: “Lau” unapopatwa na jambo.  

 

3-Sababu kufanya hivyo kunafungua njia ya ‘amali za shaytwaan.

 

4-Mwongozo wa mawazo na matamshi mazuri.

 

5-Himizo la kufanya ‘amali njema zenye manufaa (Aakhirah) na wakati huohuo kuomba msaada kutoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى).

 

6-Kufanya kinyume chake (yaani kutokutafuta manufaa yenye manufaa na kutaka msaada kutoka kwa asiyekuwa Allaah (سبحانه وتعالى) kumekatazwa, na hivyo ni ajizi. 

 

 

 

Share