58-Kitaab At-Tawhiyd: Makatazo Ya Kutukana Upepo
Mlango Wa 58
بَابٌ اَلنَّهْيُ عَنْ سَبِّ اَلرِّيحِ
Makatazo Ya Kutukana Upepo
عَنْ أُبَيِّ بْنِ كَعْبٍ (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ) أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم) قَالَ ((لاَ تَسُبُّوا اَلرِّيحَ، فَإِذَا رَأَيْتُمْ مَا تَكْرَهُونَ فَقُولُوا: اَللَّهُمَّ إِنَّا نَسْأَلُكَ مِنْ خَيْرِ هَذِهِ اَلرِّيحِ وَخَيْرِ مَا فِيهَا وَخَيْرِ مَا أُمِرَتْ بِهِ، وَنَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ هَذِهِ اَلرِّيحِ وَشَرِّ مَا فِيهَا وَشَرِّ مَا أُمِرَتْ بِه)) صَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ
Na Imepokelewa kutoka kwa Ubayy bin Ka’b (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Msitukane upepo. Mtakapoona mnalochukia semeni: “Allaahumma Nas-aluka min khayri haadhihir-riyh wa khayri maa fiyhaa, wa khayri maa umirat bihi. Wa na’uwdhu Bika min sharri haadhihir-riyh wa sharri maa fiyhaa wa sharri maa umirat bih – Ee Allaah tunakuomba khayr za upepo huu na khayr zilokuwemo ndani yake, na khayr ya vile ulioamrishwa kuvileta. Na Tunajikinga Kwako na shari za upepo huu, na shari zilokuwemo ndani yake na shari ya vile ulivyoamrishwa kuvileta”)) [At-Tirmidhiy ameikiri ni Swahiyh]
Masuala Muhimu Yaliyomo:
1-Kulaani (au kutukana) upepo kumekatazwa.
2-Mwongozo wa du’aa ya manufaa pindi mtu anapoona asiyoyapenda.
3-Upepo unakwenda kwa amri ya Allaah (سبحانه وتعالى).
4-Upepo unaweza kuamrishwa na Allaah (سبحانه وتعالى) kuleta manufaa au madhara.