59-Kitaab At-Tawhiyd: Haijuzu Kumwekea Allaah Dhana Mbaya
Mlango Wa 59
باب: يَظُنُّونَ بِاللَّـهِ غَيْرَ الْحَقِّ ظَنَّ الْجَاهِلِيَّةِ...
Haijuzu Kumwekea Allaah Dhana Mbaya
وَقَوْلُ اَللَّهِ تَعَالَى:
Na kauli ya Allaah Ta’aalaa:
يَظُنُّونَ بِاللَّـهِ غَيْرَ الْحَقِّ ظَنَّ الْجَاهِلِيَّةِ ۖ يَقُولُونَ هَل لَّنَا مِنَ الْأَمْرِ مِن شَيْءٍ ۗ قُلْ إِنَّ الْأَمْرَ كُلَّهُ لِلَّـهِ ۗ يُخْفُونَ فِي أَنفُسِهِم مَّا لَا يُبْدُونَ لَكَ ۖ يَقُولُونَ لَوْ كَانَ لَنَا مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ مَّا قُتِلْنَا هَاهُنَا ۗ قُل لَّوْ كُنتُمْ فِي بُيُوتِكُمْ لَبَرَزَ الَّذِينَ كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقَتْلُ إِلَىٰ مَضَاجِعِهِمْ ۖ وَلِيَبْتَلِيَ اللَّـهُ مَا فِي صُدُورِكُمْ وَلِيُمَحِّصَ مَا فِي قُلُوبِكُمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿١٥٤﴾
((Wakamdhania Allaah pasi na haki dhana ya kijahili; wanasema: “Je, tuna amri yoyote sisi katika jambo hili?” Sema: “Hakika amri yote ni ya Allaah.” Wanaficha katika nafsi zao yale wasiyokubainishia. Wanasema: “Lau tungelikuwa tuna amri yoyote katika jambo basi tusingeliuliwa hapa.” Sema: “Lau mngelikuwa majumbani mwenu, bila shaka wangejitokeza wale walioandikiwa kuuwawa kwenye mahali pa kuangukia wafe.” Ili Allaah Ayajaribu yale yaliyomo katika vifua vyenu na Atakase yale yaliyomo katika nyoyo zenu. Na Allaah ni Mjuzi kwa yaliyomo vifuani)) [Aal-‘Imraan (3: 154)]
وَقَوْلُهُ:
Na kauli Yake:
الظَّانِّينَ بِاللَّـهِ ظَنَّ السَّوْءِ ۚ عَلَيْهِمْ دَائِرَةُ السَّوْءِ ۖ وَغَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ وَلَعَنَهُمْ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَهَنَّمَ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا ﴿٦﴾
((Wanaomdhania Allaah dhana ovu. Utawafikia mgeuko mbaya; na Allaah Awaghadhibikie, na Awalaani, na Awaandalie Jahannam, na paovu palioje mahali pa kuishia)) [Al-Fat-h (48: 6)]
قَالَ اِبْنُ الْقَيِّمِ فِي الآيَةِ الأُولَى: فُسِّرَ هَذَا اَلظَّنُّ بِأَنَّهُ سُبْحَانَهُ لاَ يَنْصُرُ رَسُولَهُ وَأَنَّ أَمْرَهُ سَيَضْمَحِلُّ وَفُسِّرَ بِأَنَّ مَا أَصَابَهُ لَمْ يَكُنْ بِقَدَرِ اَللَّهِ وَحِكْمَتِهِ. فَفُسِّرَ بِإِنْكَارِ الْحِكْمَةِ وَإِنْكَارِ الْقَدَرِ وَإِنْكَارٍ أَنْ يُتِمَّ أَمْرَ رَسُولِهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) وَأَنْ يُظْهِرَهُ عَلَى اَلدِّينِ كُلِّه.
Ibn Al-Qayyim amesema kuhusu Aayah ya kwanza: “Dhana za kijahili ni kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Hatomnusuru Rasuli Wake, na kwamba ujumbe Wake utashindwa na kutoweka. Dhana za kijahili pia ina maana misiba iliyompata Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) haikumpata kutokana na Qadar na hikmah ya Allaah (سبحانه وتعالى). Kwa hiyo dhana kama hizo zinapeleka kukanusha Qadar na hikmah ya Allaah (سبحانه وتعالى) na kutotarajia kwamba Ujumbe wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ungekamilika na ungezishinda dini zengine zote.
وَهَذَا هُوَ ظَنُّ اَلسَّوْءِ اَلَّذِي ظَنَّهُ الْمُنَافِقُونَ وَالْمُشْرِكُونَ فِي سُورَةِ الْفَتْحِ. وَإِنَّمَا كَانَ هَذَا ظَنُّ اَلسُّوءِ لأَنَّهُ ظَنُّ غَيْرِ مَا يَلِيقُ بِهِ سُبْحَانَهُ وَمَا يَلِيقُ بِحِكْمَتِهِ وَحَمْدِهِ وَوَعْدِهِ اَلصَّادِقِ .
Hizo ndizo dhana mbaya za wanafiki na washirikina waliotajwa katika Suwrah Al-Fat-h kuwa ni ‘suw-udh-dhwann’ (dhana mbaya), na dhana mbaya haistahiki kwa Allaah (سبحانه وتعالى) Aliyetakasika na kila ovu na Mwenye Sifa zote za ukamilifu. Wala haistahiki katika hikmah Yake na kuhimidiwa Kwake wala ahadi Yake ya kweli.
فَمَنْ ظَنَّ أَنَّهُ يُدِيلُ الْبَاطِلَ عَلَى الْحَقِّ إِدَالَةً مُسْتَقِرَّةً يَضْمَحِلُّ مَعَهَا الْحَقُّ أَوْ أَنْكَرَ أَنَّ مَا جَرَى بِقَضَائِهِ وَقَدَرِهِ أَوْ أَنْكَرَ أَنْ يَكُونَ قَدَرُهُ لِحِكْمَةٍ بَالِغَةٍ يَسْتَحِقُّ عَلَيْهَا الْحَمْدَ بَلْ زَعَمَ أَنَّ ذَلِكَ لِمَشِيئَةٍ مُجَرَّدَةٍ: فَ ((ذَٰلِكَ ظَنُّ الَّذِينَ كَفَرُوا ۚ فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ كَفَرُوا مِنَ النَّارِ))
Basi atakayedhania kwamba ubatilifu (shirki, kufru, shaytwaan na upotofu wote) utashinda na kuendelea dhidi ya haki (Uislamu, Tawhiyd n.k.), au akakanusha kwamba mambo hutokea kwa Qadhwaa na Qadar (Yaliyohukumiwa na Yaliyokadiriwa), au akakanusha kwamba Ameyakadiria kwa hikmah kubwa inayostahiki kusifiwa (na kushukuriwa), au akadai kwamba hayo hutokea kwa sudfa tu, basi ((Hiyo ndio dhana ya wale waliokufuru. Basi ole wale waliokufuru kwa moto utakaowapata)) [Swaad (38: 27)]
وَأَكْثَرُ اَلنَّاسِ يَظُنُّونَ بِاَللَّهِ ظَنَّ اَلسَّوْءِ فِيمَا يَخْتَصُّ بِهِمْ وَفِيمَا يَفْعَلُهُ بِغَيْرِهِمْ وَلاَ يَسْلَمُ مِنْ ذَلِكَ إِلاَّ مَنْ عَرَفَ اَللَّهَ وَأَسْمَاءَه وَصِفَاتِهِ وَمُوجَبَ حِكْمَتِهِ وَحَمْدِهِ.
Na watu wengi wanamdhania Allaah dhana mbaya katika yanayowasibu wao wenyewe na yanayowasibu wengine. Hakuna anayesalimika na hayo isipokuwa ambaye amemtambua Allaah kwa Majina Yake Mazuri na Sifa Zake, na mujibu wa hikmah Zake na kuhimidiwa Kwake.
فَلْيَعْتَنِ اَللَّبِيبُ اَلنَّاصِحُ لِنَفْسِهِ بِهَذَا وَلْيَتُبْ إِلَى اَللَّهِ وَلْيَسْتَغْفِرْهُ مِنْ ظَنِّهِ بِرَبِّهِ ظَنَّ اَلسَّوْءِ.
Basi mwenye akili na busara achunguze nafsi yake katika mas-alah haya, na atubie kwa Allaah, na aombe maghfirah kutokana dhana mbaya kuhusu Rabb wake.
وَلَوْ فَتَّشْتَ مَنْ فَتَّشْتَّ لَرَأَيْتُ عِنْدَهُ تَعَنُّتًا عَلَى الْقَدَرِ وَمَلَامَةً لَهُ وَأَنَّهُ كَانَ يَنْبَغِي أَنْ يَكُونَ كَذَا وَكَذَا فَمُسْتَقِلٌّ وَمُسْتَكْثِرٌ.
Lau kama ungelichunguza (mtu kama huyo) ungemwona yuko katika ushupavu na ameudhika kuhusu Qadar ya Allaah (سبحانه وتعالى) akilaumu na kuinasibisha na makosa akiwaza kuwa: “Bora ingelikuwa kadhaa wa kadhaa.” Katika mtihani huu wako walioathirika kidogo na wengine kwa kuzidi mipaka.
وَفَتِّشْ نَفْسَكَ هَلْ أَنْتَ سَالِمٌ؟ فَإِنْ تَنْجُ مِنْهَا تَنْجُ مِنْ ذِي عَظِيمَةٍ وَإِلاَّ فَإِنِّي لاَ إِخَالُكَ نَاجِيًا
Chunguza nafsi yako. Je, wewe umesalimika na dhana mbaya kama hizo? Ikiwa umesalimika, basi umenusurika na balaa kubwa, laa sivyo basi hakika sidhanii kama umeokoka.
Masuala Muhimu Yaliyomo:
1-Tafsiri ya Aayah Suwrah Aal-‘Imraan (3: 154).
2-Tafsiri ya Aayah Suwrah Al-Fat-h (48: 6).
3-Tambua kuwa dhana mbaya kwa Allaah (سبحانه وتعالى) ni aina nyingi.
4-Anayetambua (maana halisi ya) Majina na Sifa za Allaah (سبحانه وتعالى) ndiye pekee aliyesalimika na dhana mbaya kuhusu Allaah (سبحانه وتعالى).