60-Kitaab At-Tawhiyd: Wanaokanusha Al-Qadar (Kudura Ya Allaah)

Mlango Wa 60

بَابٌ مَا جَاءَ فِي مُنْكِرِي الْقَدَرِ

Wanaokanusha Al-Qadar (Kudura Ya Allaah)


 

وَقَالَ اِبْنُ عُمَرَ: وَاَلَّذِي نَفْسُ اِبْنِ عُمَرَ بِيَدِهِ ، لَوْ كَانَ لأَحَدِهِمْ مِثْلُ أُحُدٍ ذَهَبًا ثُمَّ أَنْفَقَهُ فِي سَبِيلِ اَللَّهِ، مَا قَبِلَهُ اَللَّهُ مِنْهُ حَتَّى يُؤْمِنَ بِالْقَدَرِ. ثُمَّ اِسْتَدَلَّ بِقَوْلِ اَلنَّبِيِّ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((الإِيمَانُ: أَنْ تُؤْمِنَ بِاَللَّهِ وَمَلائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ وَالْيَوْمِ الآخِرِ وَتُؤْمِنَ بِالْقَدَرِ خَيْرِهِ وَشَرِّهِ)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ .

Na Ibn ‘Umar amesema: “Naapa kwa Ambaye nafsi ya Ibn ‘Umar imo Mkononi Mwake! Lau mmoja wenu angekuwa na dhahabu mfano wa jabali la Uhud, kisha akaitoa katika njia ya Allaah, basi Allaah Asingeipokea mpaka iwe ameamini Qadar (Makadirio ya Allaah)” Kisha akatoa dalili kwa kauli ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): ((Iymaan ni kumwamini Allaah, na Malaika Wake, na Vitabu Vyake, na Mitume Wake, Na Siku ya mwisho, na kuamini Qadar khayr yake na shari yake)) [Muslim]

 

وَعَنْ عُبَادَةَ بنِ اَلصَّامِتِ: أَنَّهُ قَالَ لابْنِهِ: يَا بُنَيَّ إِنَّكَ لَنْ تَجِدَ طَعْمَ الإِيمَانِ حَتَّى تَعْلَمَ أَنَّ مَا أَصَابَكَ لَمْ يَكُنْ لِيُخْطِئَكَ، وَمَا أَخْطَأَكَ لَمْ يَكُنْ لِيُصِيبَكَ. سَمِعْتُ رَسُولَ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)  يَقُولُ: ((إِنَّ أَوَّلَ مَا خَلَقَ اَللَّهُ الْقَلَمَ، فَقَالَ لَهُ: اُكْتُبْ!  فَقَالَ: رَبِّ وَمَاذَا أَكْتُبُ؟ قَالَ: اُكْتُبْ مَقَادِيرَ كُلِّ شَيْءٍ حَتَّى تَقُومَ اَلسَّاعَةُ)) يَا بُنَيَّ: سَمِعْتُ رَسُولَ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) يَقُولُ:  ((مَنْ مَاتَ عَلَى غَيْرِ هَذَا فَلَيْسَ مِنِّي))

Na Imepokelewa kutoka kwa ‘Ubaadah bin Swaamit kwamba amemwambia mwanawe: “Ee mwanangu! Hakika hutapata ladha ya iymaan mpaka utambue kwamba kilichokusibu kisingekukosa, na kilichokukosa kisingekupata; Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Kitu cha mwanzo Allaah kuumba ni kalamu. Kisha Akaiambia: Andika! [Kalamu] ikasema: “Rabb wangu, niandike nini?” Akasema: Andika makadirio ya kila kitu mpaka siku itakayosimama Saa [Qiyaamah])). Ee mwanangu! Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Atakayefariki kinyume na haya, basi si miongoni mwangu)).

 

وَفِي رِوَايَةٍ لأَحْمَدَ: ((إِنَّ أَوَّلَ مَا خَلَقَ اَللَّهُ تَعَالَى الْقَلَمَ فَقَالَ لَهُ:  اُكْتُبْ! فَجَرَى فِي تِلْكَ اَلسَّاعَةِ بِمَا هُوَ كَائِنٌ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ))   

Na katika riwaayah ya Imaam Ahmad: ((Kitu cha mwanzo Allaah kukiumba ni kalamu. Akaiambia: Andika! Na katika saa hiyo, [yakaandikwa] yote yatakayotokea mpaka Siku ya Qiyaamah))

 

وَفِي رِوَايَةٍ لابْنِ وَهْبٍ قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم): ((فَمَنْ لَمْ يُؤْمِنْ بِالْقَدَرِ خَيْرِهِ وَشَرِّهِ أَحْرَقَهُ اَللَّهُ بِالنَّار))

Na katika riwaayah ya Ibn Wahb amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Basi asiyeamini Qadar; khayr zake na shari zake, Allaah Atamuunguza motoni))

 

وَفِي الْمُسْنَدِ  وَ اَلسُّنَنِ عَنِ ابْنِ الدَّيْلَمِيِّ: قَالَ: أَتَيْتُ أُبَيَّ بْنَ كَعْبٍ، فَقُلْتُ فِي نَفْسِي شَيْءٌ مِنَ الْقَدَرِ. فَحَدِّثْنِي بِشَيْءٍ لَعَلَّ اَللَّهَ يُذْهِبُهُ مِنْ قَلْبِي، فَقَالَ: لَوْ أَنْفَقْتَ مِثْلَ أُحُدٍ ذَهَبًا مَا قَبِلَهُ اَللَّهُ مِنْكَ حَتَّى تُؤْمِنَ بِالْقَدَرِ، وَتَعْلَمَ أَنَّ مَا أَصَابَكَ لَمْ يَكُنْ لِيُخْطِئَكَ وَمَا أَخْطَأَكَ لَمْ يَكُنْ لِيُصِيبَكَ، وَلَوْ مِتَّ عَلَى غَيْرِ هَذَا، لَكُنْتَ مِنْ أَهْلِ اَلنَّارِ. قَالَ: فَأَتَيْتُ عَبْدَ اَللَّهِ بْنَ مَسْعُودٍ وَحُذَيْفَةَ بْنَ الْيَمَانِ وَزَيْدَ بْنَ ثَابِتٍ فَكُلُّهُمْ حَدَّثَنِي بِمِثْلِ ذَلِكَ عَنْ اَلنَّبِيِّ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) حَدِيثٌ صَحِيحٌ رَوَاهُ الْحَاكِمُ فِي "صَحِيحِهِ

Na imenukuliwa katika Musnad ya Ahmad na Sunan Abiy Daawuwd kutoka kwa Ibn Ad-Daylamiyy amesema: Nilimwendea Ubayy bin Ka’b nikasema: “Nina kitu (shaka)] katika nafsi yangu kuhusu Qadar. Nihadithie chochote huenda Allaah Ataiondosha (shaka) moyoni mwangu.” Akasema: “Lau kama utatoa dhahabu mfano wa jabali la Uhud, Allaah Hatoikubali kwako mpaka uamini Qadr, na  utambue kwamba kilichokusibu kisingekukosa na kilichokukosa kisingekupata. Na lau ukifariki kinyume chake, bila shaka utakuwa miongoni mwa watu wa motoni” Akasema: “Nikamwendea ‘Abdullaahi bin Mas’uwd, Hudhayfah bin Al-Yamaani na Zayd bin Thaabit, na wote wakanihadithia kama hivyo alivyosema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)” [Hadiyth Swahiyh ameipokea Al-Haakim katika Swahiyh yake]

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

 

1-Maelezo ya wajibu wa kuamini Al-Qadar.

 

2- Maelezo ya maana ya kuiamini.

 

3-Kubatilika ‘amali za asiyeiamini.

 

4-Hakuna atakayepata ladha ya iymaan isipokuwa mpaka aamini Al-Qadar.

 

5-Kutajwa kilichoumbwa kwanza na Allaah (سبحانه وتعالى).

 

6-Kalamu imeshaandika yote yatakayokuja mpaka Siku ya Mwisho.

 

7-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kumkataa yeyote asiyeamini Al-Qadar.

 

8-Tabia ya As-Salaf kuwauliza wenye ujuzi kuhusu yale wasiyo na hakika nayo ili kuondoa shaka.

 

9- Wanachuoni Waislamu walijibu majibu yaliyoondoa shaka zote kuhusu Qadar kwa kunukuu kauli za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم).

 

 

 

Share