61-Kitaab At-Tawhiyd: Wachoraji Picha Za Viumbe Wachongaji Masanamu Vinyago n.k.

Mlango Wa 61

بَابٌ مَا جَاءَ فِي الْمُصَوِّرِينَ

Wachoraji Picha Za Viumbe Wachongaji Masanamu Vinyago n.k.


 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((قَالَ اللهُ تَعَالَى: وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنْ ذَهَبَ يَخْلُقُ كَخَلْقِي؛ فَلْيَخْلُقُوا ذَرَّةً، أَوْ لِيَخْلُقُوا حَبَّةً، أَوْ لِيَخْلُقُوا شَعِيْرَةً ))  أَخْرَجَاهُ

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Allaah Aliyetukuka Amesema: Nani dhalimu zaidi kuliko anayejaribu kuumba kama kuumba Kwangu? Basi na waumbe chembe moja au waumbe punje ya nafaka, au waumbe chembe ya shayiri)) [Al-Bukhaariy na Muslim]  

 

وَلَهُمَا عَنْ عَائِشَةَ (رَضِيَ اللهُ عَنْهَا) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم) قَال: ((أَشَدُّ النَّاسِ عَذَابًا يَوْمَ القِيَامَةِ الَّذِينَ يُضَاهِئُونَ بِخَلْقِ اللَّهِ))

Nao (Al-Bukhaariy na Muslim) wamesimulia kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللهُ عَنْهَا) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Watakaokuwa na adhabu kali Siku ya Qiyaamah ni wanaomuiga Allaah katika uumbaji Wake))

 

 وَلَهُمَا عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ (رضي الله عنهما) :  سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) يَقُولُ: ((كُلُّ مُصَوِّرٍ فِي النَّارِ يُجْعَلُ لَهُ بِكُلِّ صُورَةٍ صَوَّرَهَا نَفْسٌ يُعَذَّبُ بِهَا فِي جَهَنَّمَ))

Nao (Al-Bukhaariy na Muslim) wamesimulia kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Kila mchoraji picha atakuwa motoni. Kila picha aliyoichora, itatiwa roho nayo itamuadhibu katika Jahannam))

 

وَلَهُمَا عَنْهُ مَرْفُوعًا: ((مَنْ صَوَّرَ صُورَةً فِي الدُّنْيَا كُلِّفَ أَنْ يَنْفُخَ فِيهَا الرُّوحَ وَلَيْسَ بِنَافِخٍ))

Nao (Al-Bukhaariy na Muslim) wamesimulia kutoka kwake pia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) Hadiyth Marfuw’: ((Atakayechora picha duniani atalazimishwa aitie roho (Siku ya Qiyaamah), na wala hatoweza))

 

وَلِمُسْلِمٍ عَنْ أَبِي الهَيَّاجِ قَالَ: قَالَ لِي عَلِيٌّ: أَلاَ أَبْعَثُكَ عَلَى مَا بَعَثَنِي عَلَيْهِ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)؟: أَلاَّ تَدَعَ صُورَةً إِلاَّ طَمَسْتَهَا وَلاَ قَبْرًا مُشْرِفًا إِلاَّ سَوَّيْتَهُ  

Na Muslim amesimulia kutoka kwa Abuu Al-Hayyaaj amesema: ‘Aliyy ameniambia: “Je, nikutume lile alilonituma Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)?  Kwamba: Usibakishe sura (picha, sanamu, kinyago) yoyote ila uiharibu, wala kaburi lilonyanyuliwa ila (ulibomoe na) ulisawazishe.”

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

 

1-Karipio kali kwa wenye kuchora (na kutengeneza, kuchonga) picha, masanamu, vinyago n.k.

 

2-Imekaripiwa vikali kwa sababu watengenezaji na wachoraji picha hawamuheshimu vilivyo Allaah (سبحانه وتعالى) kama Alivyosema Yeye Mwenyewe: ((Nani dhalimu zaidi kuliko anayejaribu kuumba kama kuumba Kwangu?)).

 

3-Tanbihi ya nguvu kutofuatisha uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) katika kuumba na ule wa wengine kama unavyoashiria katika kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى): ((Basi na waumbe chembe moja au waumbe punje ya nafaka, au waumbe chembe ya shayiri)).

 

4-Tangazo kuwa wachoraji, watengenezaji picha wataadhibiwa vikali zaidi (Siku ya Qiyaamah).  

 

5-Allaah (سبحانه وتعالى) Ataumba roho katika kila picha (sanamu, kinyago n.k.) nayo itamuadhibu mwenye kuzitengeneza katika moto wa Jahannam.

 

6-Wafanya picha wataambiwa wazitie roho (uhai) picha zao.

 

7-Amri ya kuziharibu picha, vinyago, masanamu n.k. popote zitakapoonekana. (Pia kusawazisha makaburi yaliyonyanyuliwa).  

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share