64-Kitaab At-Tawhiyd: Kuapa Kwamba Allaah Hatafanya Jambo Fulani

Mlango Wa 64

بَابٌ  :مَا جَاءَ فِي الإِقْسَامِ عَلَى اللَّهِ

Kuapa Kwamba Allaah Hatafanya Jambo Fulani


 

 

عَنْ جُنْدُبِ بنِ عَبْدِ اللَّهِ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ ((صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)): ((قَالَ رَجُلٌ: وَاللَّهِ لاَ يَغْفِرُ اللَّهُ لِفُلانٍ. فَقَالَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ: مَنْ ذَا الَّذِي يَتَأَلَّى عَلَيَّ أَنْ لاَ أَغْفِرَ لِفُلانٍ؟ إِنِّي قَدْ غَفَرْتُ لَهُ وَأَحْبَطْتُ عَمَلَكَ)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Imepokelewa kutoka kwa Jundub bin ‘Abdillaah   (رضي الله عنه)amesema: “Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم ) amesema: ((Mtu mmoja alisema: Wa-Allaahi Allaah Hatomghufuria fulani! Allaah (عزّ وجلّ) Akasema: Ni nani huyo anayeniamulia kuwa Sitomghufuria fulani? Mimi Nimeshamghufuria fulani na Nimebatilisha ‘amali zako)) [Muslim]  

 

وَفِي حَدِيثِ أَبِي هُرَيْرَةَ : أَنَّ "القَائِلَ رَجُلٌ عَابِدٌ" قَالَ أَبُو هُرَيْرَةَ : تَكَلَّمَ بِكَلِمَةٍ، أَوْبَقَتْ دُنْيَاهُ وَآخِرَتَهُ

Na katika Hadiyth ya Abuu Hurayrah (رضي الله عنه)  kwamba: Mtu aliyesema hivyo ni mshika ‘ibaadah. Abuu Hurayrah akasema: “Ametamka neno moja lilomharibia duniya na Aakhirah yake”

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

 

1-Onyo dhidi ya kutokuapa kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Hatafanya jambo fulani.

 

2-Moto wa Jahannam uko karibu nasi kuliko kamba za viatu.

 

3-Kadhalika Jannah.

 

4-Maelezo kuwa wakati mwingine, mwana Aadam hutamka maneno pasi na kukusudia lakini athari zake ni kubwa mno kiasi ya kumuangamiza kama ilivyo katika Hadiyth:

 

عن أَبي عبد الرحمن بِلالِ بن الحارِثِ المُزَنِيِّ رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ : ((إنَّ الرَّجُلَ لَيَتَكَلَّمُ بِالكَلِمَةِ مِنْ رِضْوَانِ اللهِ تَعَالَى مَا كَانَ يَظُنُّ أنْ تَبْلُغَ مَا بَلَغَتْ يَكْتُبُ اللهُ لَهُ بِهَا رِضْوَانَهُ إِلَى يَومِ يَلْقَاهُ ، وإنَّ الرَّجُلَ لَيَتَكَلَّمُ بِالكَلِمَةِ مِنْ سَخَطِ اللهِ مَا كَانَ يَظُنُّ أنْ تَبْلُغَ مَا بَلَغَتْ يَكْتُبُ الله لَهُ بِهَا سَخَطَهُ إِلَى يَوْمِ يَلْقَاهُ )). رواه مالك في المُوَطَّأ ، والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

 

Abuu 'Abdir-Rahmaan Bilaal bin Al-Haarith Al-Muzniy (رضي الله عنه)  amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: ((Kwa hakika mja atazungumza neno linalomridhisha Allaah, wala asidhani kuwa litafikia lilipofikia, Allaah Amuandikie kwa neno hilo Radhi Zake hadi Siku ya Qiyaamah. Na Kwa hakika mja atazungumza neno linalomkasirisha Allaah, wala asidhani kuwa litafikia lilipofikia, Allaah Amuandikie kwa neno hilo hasira Zake hadi Siku ya Qiyaamah)) [Maalik katika Muwattwa na At-Tirmidhiy ambaye amesema Hadiyth hii ni Hasan Swahiyh]

 

5-Wakati mwingine, mwana Aadam husamehewa dhambi zake zote kwa jambo alichukialo sana.

 

 

 

 

 

Share