65-Kitaab At-Tawhiyd: Haiombwi Shafaa-ah Ya Allaah Juu Ya Viumbe Vyake
Mlango Wa 65
بَابٌ لَا يُسْتَشْفَعُ بِاَللَّهِ عَلَى خَلْقِهِ
Haiombwi Shafaa-ah Ya Allaah Juu Ya Viumbe Vyake
عَنْ جُبَيْرِ بْنِ مُطْعِمٍ (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ) قَالَ : جَاءَ أَعْرَابِيٌّ إِلَى اَلنَّبِيِّ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فَقَالَ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! نُهِكَتِ الأَنْفُسُ وَجَاعَ الْعِيَالُ وَهَلَكَتِ الأَمْوَالُ فَاسْتَسْقِ لَنَا رَبَّكَ، فَإِنَّا نَسْتَشْفِعُ بِاَللَّهِ عَلَيْكَ، وَبِكَ عَلَى اَللَّهِ. فَقَالَ اَلنَّبِيُّ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((سُبْحَانَ اَللَّهِ! سُبْحَانَ اَللَّهِ!)) فَمَا زَالَ يُسَبِّحُ حَتَّى عُرِفَ ذَلِكَ فِي وُجُوهِ أَصْحَابِهِ ثُمَّ قَالَ: ((وَيْحَكَ! أَتَدْرِي مَا اَللَّهُ؟ إِنَّ شَأْنَ اَللَّهِ أَعْظَمُ مِنْ ذَلِكَ، إِنَّهُ لاَ يُسْتَشْفَعُ بِاَللَّهِ عَلَى أَحَدٍ مِنْ خَلْقِهِ)) وَذَكَرَ الْحَدِيثَ رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ
Imepokelewa kutoka kwa Jubayr bin Mutw’-im(رضي الله عنه) amesema: Alikuja Bedui kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Watu wanaangamia, na watoto wana njaa, mali imeangamia [mimea na wanyama], basi muombe Rabb wako Atuletee mvua, kwani tunaomba shafaa’ah ya Allaah kwako na shafaa’ah yako kwa Allaah.” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Subhaana-Allaah! Subhaana Allaah!)). Akaendelea kumtakasa Allaah mpaka athari yake ikadhihiri nyusoni mwa Maswahaba. Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Ole wako! Unamjua nani Allaah? Hakika Utukufu wa Allaah ni adhimu zaidi kuliko hilo! Haiombwi shafaa’ah ya Allaah juu ya yeyote kati ya viumbe Wake)) [Akataja Hadiyth Abuu Daawuwd]
Masuala Muhimu Yaliyomo:
1-Nabiy kukaripia kunaposemwa: “Tunaomba shafaa’ah ya Allaah kwako.”
2-Ghadhabu ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ilidhihirika kwa Maswahaba (رضي الله عنهم).
3-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakukemea ombi la shafaa’ah yake kwa Allaah.
4-Maana ya Subhana-Allaah. (Allaah (سبحانه وتعالى) Yuko juu kabisa ya viumbe Vyake na Ametakasika kabisa dhidi ya ila na hahitaji lolote].
5-Waislamu walimuomba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aombe mvua.