002-Aayah Na Mafunzo: Aina Mbili Za Hidaaya

 

 Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Aina Mbili Za Hidaaya

 

 

ذَٰلِكَ الْكِتَابُ لَا رَيْبَ ۛ فِيهِ ۛ هُدًى لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٢﴾

2. Hiki ni Kitabu kisicho na shaka ndani yake, ni Mwongozo kwa wenye taqwa.

 

Mafunzo:

 

Hudaa, Hidaayah ziko aina mbili;

 

1- Hidaayatut-Tawfiyq:

 

Ni iymaan ambayo mahali pake ni moyoni na ni Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Pekee Awezaye kuiweka katika nyoyo za waja. Dalili ni kauli yake Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa)  Alipomwambia Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye alipendelea kumuongoza ‘Ammi yake Abuu Twaalib katika Uislamu alipokuwa anakaribia kuaga dunia. Allaah Akasema:

 

إِنَّكَ لَا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ ﴿٥٦﴾

56. Hakika wewe huwezi kumhidi umpendaye; lakini Allaah Humhidi Amtakaye, Naye Anawajua zaidi wenye kuongoka.” [Al-Qaswasw (28: 56)].

 

Na mfano pia Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

فَإِنَّ اللَّـهَ يُضِلُّ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ ۖ

Basi hakika Allaah Anampotoa Amtakaye na Anamhidi Amtakaye [Faatwir: 8]

 

 

2-Hidaayatul-Irshaad (hidaaya ya kuongoza):

 

Ni kuelekeza, kubainisha, kuongoza njia, kumwongoza mtu katika kutekeleza mema n.k. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

وَإِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٥٢﴾

Na hakika wewe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) bila shaka unaongoza kuelekea njia iliyonyooka. [Ash-Shuwraa (42 :52)].

 

Na mfano kauli Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

وَأَمَّا ثَمُودُ فَهَدَيْنَاهُمْ فَاسْتَحَبُّوا الْعَمَىٰ عَلَى الْهُدَىٰ فَأَخَذَتْهُمْ صَاعِقَةُ الْعَذَابِ الْهُونِ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿١٧﴾

Na ama kina Thamuwd, Tuliwaongoza, lakini walistahabu upofu kuliko Uongofu. [Fusw-Swilat: 18]

 

 

 

Share