003-Aayah Na Mafunzo: Maana Ya Kusimamisha Swalaah
Aayah Na Mafunzo
Al-Baqarah
Maana Ya Kusimamisha Swalaah
الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِالْغَيْبِ وَيُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ﴿٣﴾
3. Ambao huamini ya ghayb na husimamisha Swalaah na katika vile Tulivyowaruzuku hutoa.
Mafunzo:
Maana ya kusimamisha Swalaah: Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: “Ni kuswali kwa kuzingatia nguzo na sharti zake.” Adhw-Dhwahaak amesema kuwa Ibn ‘Abbaas alisema: “Iqamaat Asw-Swalaah maana yake ni kukamilisha rukuu, sujuwd, kusoma Qur-aan, khushuu (unyenyekevu), na kuhudhurisha moyo katika Swalaah.” Qataadah alisema: “Iqamaat Asw-Swalaah maana yake ni kuchunga wakati, wudhuu, rukuu na sujuwd za Swalaah.” Muqaatil bin Hayyaan alisema: “Iqaamat Asw-Swalaah ina maana: Kuchunga wakati, kujitwaharisha kwa ajili yake, kukamilisha rukuu, sujuwd na kusoma Qur-aan, tashahhud na kumwombea rahmah Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Hiyo ndiyo Iqaamat Asw-Swalaah.” [Tafsiyr Ibn Kathiyr]