029-Aayah Na Mafunzo: 'Aqiydah Ya Salaf Kuhusu Maana ya Istiwaa

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

'Aqiydah Ya Salaf Kuhusu Maana ya Istiwaa

 

 

هُوَ الَّذِي خَلَقَ لَكُم مَّا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ فَسَوَّاهُنَّ سَبْع سَمَاوَاتٍ ۚ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٢٩﴾ 

29. Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbieni vyote vilivyomo ardhini kisha Istawaakuzielekea mbingu na Akazifanya timilifu mbingu saba, Naye kwa kila kitu ni Mjuzi.

 

Mafunzo:

 

 

Istawaa: Inamaanisha Yuko juu kabisa kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa)

 

Faida: Msimamo wa Salaf katika tafsiyr ya Aayah hiyo ni kama uliopokelewa kuwa, Ja’far bin ‘Abdillaah na wengine miongoni mwao walisema: “Tulikuwa kwa Imaam Maalik bin Anas basi akatokea mtu akamuuliza? Ee Abaa ‘Abdillaah! Allaah (Ta’aalaa) Anasema:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ ﴿٥﴾

Mwingi wa rahmah juu ya ‘Arshi Istawaa. [Twaaha  (20: 5)]. 

 

Je, vipi Istawaa? Basi Imaam Maalik hakuwahi kughadhibika kutokana na kitu chochote kile kama alivyoghadhibika kutokana na swali la mtu huyo, kisha [Imaam Maalik] akatazama chini na huku akikwaruzakwaruza kwa kijiti kilichokuwa kwenye mkono wake mpaka akarowa jasho, kisha akanyanyua kichwa chake na kukirembea kile kijiti kisha akasema: ‘Vipi’ ni ghayr ma’quwl (hakutambuliki), na Al-Istiwaa ghayr maj-huwl (si jambo lisilojulikana), na kuamini hilo ni waajib (lazima), na kuuliza (au kuhoji hilo) ni bid’ah (uzushi); na nina khofu kuwa wewe ni mzushi! Akaamrisha mtu huyo atolewe, basi akatolewa. [Imesimuliwa kwenye Al-Hilyah (6/325-326) na pia imesimuliwa na Abuu ‘Uthmaan Asw-Swaabuniy katika ‘Aqiydatu As-Salaf Asw-haab Al-Hadiyth uk. (17-18), kutoka kwa Ja’far bin ‘Abdillaah]

 

Share