066-Aayah Na Mafunzo: Kumuasi Allaah Katika Aliyoyaharamisha Kunastahiki Adhabu

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Kumuasi Allaah Katika Aliyoyaharamisha Kunastahiki Adhabu

 

 

فَجَعَلْنَاهَا نَكَالًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهَا وَمَا خَلْفَهَا وَمَوْعِظَةً لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٦٦﴾

66. Tukaifanya kuwa ni adhabu ya kuonya kwa waliokuweko zama zao na wataokuja baada yao na ni mawaidha kwa wenye taqwa.

 

Mafunzo:

 

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Msifanye makosa waliyoyafanya Mayahudi wakakiuka Aliyoyaharamisha Allaah kwa hila ndogo ndogo.” [Imaam Abuu ‘Abdillaah bin Batwwah; Irwaa Al-Ghaliyl (5/375) – Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

 

Share