065-Aayah Na Mafunzo: Maana Ya As-Sabt Na Mayahudi Kuvunja Shariy’ah Yake
Aayah Na Mafunzo
Al-Baqarah
Maana Ya As-Sabt Na Mayahudi Kuvunja Shariy’ah Yake
وَلَقَدْ عَلِمْتُمُ الَّذِينَ اعْتَدَوْا مِنكُمْ فِي السَّبْتِ فَقُلْنَا لَهُمْ كُونُوا قِرَدَةً خَاسِئِينَ ﴿٦٥﴾
65. Na kwa yakini mlikwishawajua wale miongoni mwenu waliotaadi mipaka ya As-Sabt Tukawaambia: “Kuweni manyani waliobezwa.”
Mafunzo:
As-Sabt maana yake asili, ni mapumziko na hivyo Siku hiyo yao ya mapumziko (Jumamosi), Mayahudi waliwekewa shariy’ah wasivue samaki lakini walikhalifu amri kwa kutumia njama na ujanja wakavua samaki kumuasi Allaah, basi Allaah Akawaghadhibikia na kuwageuza manyani.