058-Aayah Na Mafunzo: Ubadilishaji Wa Maana Ya Hittwah: Tuondolee Uzito Wa Madhambi
Aayah Na Mafunzo
Al-Baqarah
Ubadilishaji Wa Maana Ya Hittwah
وَإِذْ قُلْنَا ادْخُلُوا هَـٰذِهِ الْقَرْيَةَ فَكُلُوا مِنْهَا حَيْثُ شِئْتُمْ رَغَدًا وَادْخُلُوا الْبَابَ سُجَّدًا وَقُولُوا حِطَّةٌ نَّغْفِرْ لَكُمْ خَطَايَاكُمْ ۚ وَسَنَزِيدُ الْمُحْسِنِينَ ﴿٥٨﴾
58. Na pindi Tuliposema: “Ingieni mji huu (Quds) na kuleni humo maridhawa popote mpendapo, na ingieni katika mlango wake huku mmeinama kunyenyekea na semeni “Hittwah" (Tuondolee uzito wa madhambi); Tutakughufurieni makosa yenu na Tutawazidishia (thawabu) wafanyao ihsaan.
Mafunzo:
Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Wana wa Israaiyl waliamrishwa kuingia kupitia mlangoni huku wainame na wanyenyekee na waseme ‘Hittwah’ (Tuondolee uzito wa madhambi). Lakini waliingia kinyumenyume wakipotosha maneno wakisema: Habbat fiy sha’rah (mbegu katika unywele).” [Al-Bukhaariy]