057-Aayah Na Mafunzo: Uyoga Ni Aina Ya Manna Ni Shifaa Ya Macho
Aayah Na Mafunzo
Al-Baqarah
Uyoga Ni Aina Ya Manna Ni Shifaa Ya Macho
وَظَلَّلْنَا عَلَيْكُمُ الْغَمَامَ وَأَنزَلْنَا عَلَيْكُمُ الْمَنَّ وَالسَّلْوَىٰ ۖ كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ ۖ وَمَا ظَلَمُونَا وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ﴿٥٧﴾
57. Na Tukakufunikeni kwa mawingu na Tukakuteremshieni Al-Manna na As-Salwaa. (Tukakwambieni): “Kuleni katika vizuri Tulivyokuruzukuni.” Hawakutudhulumu Sisi lakini walikuwa wakizidhulumu nafsi zao.
Mafunzo:
Faida: Sa’iyd bin Zayd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Al-Kama-ah (uyoga) ni aina ya manna na maji yake ni shifaa (ponyo) ya macho.” [Al-Bukhaariy (4478)]