047-Aayah Na Mafunzo: Ummah Bora Ni Ummah Wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
Aayah Na Mafunzo
Al-Baqarah
Ummah Bora Ni Ummah Wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اذْكُرُوا نِعْمَتِيَ الَّتِي أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَنِّي فَضَّلْتُكُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿٤٧﴾
47. Enyi wana wa Israaiyl! Kumbukeni neema Yangu Niliyokuneemesheni na hakika Mimi Nimekufadhilisheni juu ya walimwengu wote.
Mafunzo:
Kufadhilishwa kwa hao Baniy Israaiyl juu ya walimwengu wote; makusudio yake ni walimwengu wa zama zao kwani inafahamika kuwa ummah uliokuwa bora kuliko ummah zote ni ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa dalili ya kauli ya Allaah (Ta’aalaa): “Mmekuwa ummah bora kabisa uliotolewa (mfano) kwa watu; mnaamrisha mema na mnakataza munkari na mnamwamini Allaah. Na lau wangeliamini Ahlul-Kitaabi ingelikuwa ni bora kwao, miongoni mwao wanaoamini na wengi wao ni mafasiki.” [Aal-‘Imraan (3: 110)]