081-Aayah Na Mafunzo: Madhambi Madogo Yanajikusanya Mpaka Yanaangamiza

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Madhambi Madogo Yanajikusanya Mpaka Yanaangamiza

 

 

 

بَلَىٰ مَن كَسَبَ سَيِّئَةً وَأَحَاطَتْ بِهِ خَطِيئَتُهُ فَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٨١﴾

81. Ndio! Yeyote aliyechuma uovu na yakamzunguka kwayo makosa yake; basi hao ni watu wa motoni, wao humo ni wenye kudumu.

 

 

Mafunzo:

 

Abdullaah bin Mas‘uwd  (Radhiwya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Tahadharini na madhambi madogo, kwa sababu yanajikusanya kwa mtu mpaka yanamuangamiza.” Kisha akapiga mfano: “Kama vile mfano wa watu waliopiga kambi katika ardhi tambarare kisha wakaja watumishi wao, mmoja wao akakusanya kuni na mwengine akakusanya kuni mpaka zikawa nyingi za kutosha kisha wakakoka moto na wakapika walivyovitia humo.” [Musnad Ahmad (5/312); Swahiyh Al-Jaami’ (2687)]

 

 

 

 

Share