083-Aayah Na Mafunzo: ‘Amali Bora Kabisa Kuswali Kwa Wakati Wake Kuwafanyia Wema...

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

‘Amali Bora Kabisa Kuswali Kwa Wakati Wake Kuwafanyia Wema Wazazi Na Jihaad

 

 

 

وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَ بَنِي إِسْرَائِيلَ لَا تَعْبُدُونَ إِلَّا اللَّـهَ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَقُولُوا لِلنَّاسِ حُسْنًا وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ ثُمَّ تَوَلَّيْتُمْ إِلَّا قَلِيلًا مِّنكُمْ وَأَنتُم مُّعْرِضُونَ ﴿٨٣﴾ 

83. Na pindi Tulipochukua fungamano ya wana wa Israaiyl (Tukawaambia): “Msiabudu isipokuwa Allaah; na muwafanyie ihsaan wazazi wawili, na jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini; na semeni na watu kwa uzuri na simamisheni Swalaah, na toeni Zakaah;” kisha mkakengeuka ila wachache miongoni mwenu na hali nyinyi mnapuuza.

 

 

Mafunzo:

 

Ibn Mas‘uwd  (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba: Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah, ‘amali gani bora kabisa?  Akasema: “Kuswali kwa wakati wake.”  Nikasema: Kisha ipi? Akasema: “Kuwatendea wema wazazi wawili” Nikasema: Kisha ipi? Akasema: “Jihaad katika njia ya Allaah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Share