087-Aayah Na Mafunzo: Uthibitisho Kuwa Ruwhul-Qudus Ni Jibriyl ('Alayhis-Salaam)

Aayah Na Mafunzo

 

Al-Baqarah

 

Uthibitisho Kuwa Ruwhul-Qudus Ni Jibriyl ('Alayhis-Salaam)

 

 Alhidaaya.com

 

وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ وَقَفَّيْنَا مِن بَعْدِهِ بِالرُّسُلِ ۖ وَآتَيْنَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ الْبَيِّنَاتِ وَأَيَّدْنَاهُ بِرُوحِ الْقُدُسِ ۗ أَفَكُلَّمَا جَاءَكُمْ رَسُولٌ بِمَا لَا تَهْوَىٰ أَنفُسُكُمُ اسْتَكْبَرْتُمْ فَفَرِيقًا كَذَّبْتُمْ وَفَرِيقًا تَقْتُلُونَ ﴿٨٧﴾

87. Na kwa yakini Tulimpa Muwsaa Kitabu na Tukafuatisha Rusuli baada yake. Na Tukampa ‘Iysaa mwana wa Maryam hoja bayana na Tukamtia nguvu kwa Ruwhil-Qudus (Jibriyl (عليه السلام. Je, basi kila anapokujieni Rasuli kwa yale yasiyoyapenda nafsi zenu, mlitakabari; basi kundi mlilikadhibisha na kundi mnaliua.

 

Mafunzo:

 

Uthibitisho kwamba Jibriyl (‘Alayhis-salaam) ni Ruwh Al-Qudus: ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) amehadithia kwamba: Rasuli wa Allaah alijenga minbar ndani ya Masjid ambapo Hasan bin Thaabit (mshairi maarufu) alikuwa akimtetea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) (kwa mashairi yake). Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Yaa Allaah! Msaidie Hasan kwa Ruwh Al-Qudus kama alivyomlinda Rasuli Wako.” [Al-Bukhaariy]

 

Pia, Ibn Mas‘uwd  (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Ruwh Al-Qudus alinifahamisha kuwa hakuna roho itakayokufa mpaka imalizike rizki yake na muda wake, kwa hiyo mcheni Allaah na mtakeni rizki katika hali iliyo bora.” [As-Sunnah: (14/304), ameisahihisha Al-Albaaniy katika Mushkilat Al-Faqar (15), Swahiyh Al-Jaami’ (2085) Hadiyth kutoka Abuu Umaamah Al-Baahiliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu)]

 

 

Share