172-Aayah Na Mafunzo: Du’aa Ya Mwenye Kula Haraam Haikubalilwi

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Du’aa Ya Mwenye Kula Haraam Haikubalilwi

 

www.alhidaaya.com

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ وَاشْكُرُوا لِلَّـهِ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ ﴿١٧٢﴾

172. Enyi walioamini! Kuleni vizuri Tulivyokuruzukuni na mshukuruni Allaah mkiwa mnamwabudu Yeye Pekee.

Mafunzo:

 

 

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Enyi watu! Hakika Allaah ni Mzuri na Hapokei ila kilicho kizuri. Na Allaah Amewaamrisha Waumini kama Alivyowaamrisha Rasuli Anaposema: “Enyi Rusuli! Kuleni katika vizuri na tendeni mema, hakika Mimi kwa yale myatendayo ni Mjuzi.” [Al-Muuminuwn (23: 51)] Na Anasema: “Enyi walioamini! Kuleni vizuri Tulivyokuruzukuni.” Kisha akataja kisa cha mtu aliyekuwa safarini akiwa katika hali ya uchafu na mavumbi akiinua mikono yake mbinguni akiomba: Eee Rabb! Ee Rabb! Na hali chakula chake ni haramu, kinywaji chake ni haramu na kajengeka mwili wake kwa haramu vipi atakubaliwa du'aa yake?’ [Muslim]   

 

Share