185-Aayah Na Mafunzo: Mwezi Wa Ramadhwaan Ni Mwezi Wa Qur-aan

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Mwezi Wa Ramadhwaan Ni Mwezi Wa Qur-aan

 

 www.alhidaaya.com

 

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ۖ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۗ يُرِيدُ اللَّـهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا اللَّـهَ عَلَىٰ مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿١٨٥﴾

Mwezi wa Ramadhwaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan ili iwe mwongozo kwa watu na hoja bayana za mwongozo na pambanuo (la haki na batili). Basi atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi na afunge. Na atakayekuwa mgonjwa au safarini, basi (inapaswa kulipa) idadi sawa katika masiku mengineyo. Allaah Anakutakieni mepesi na wala Hakutakieni magumu; na ili mkamilishe idadi na ili mumkabbir Allaah kwa kuwa Amekuongozeni na ili mpate kushukuru. [Al-Baqarah: 185]

 

 

Mafunzo:

 

 

“Alikuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ajwad (mkarimu) wa watu, na alikuwa ajwad zaidi katika Ramadhwaan wakati anapokutana na Jibriyl (‘Alayhis Salaam), alikuwa - Jibriyl (‘Alayhis Salaam)- akimjia Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wasallam kila usiku wa Ramadhwaan akimdurusisha Qur-aan” [Imepokelewa na Al-Bukhaariy, kitabu cha Swawm, mlango alikuwa (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mkarimu (mbora) zaidi katika Ramadhwaan, Hadiyth namba 1179]

 

Share