191-Aayah Na Mafunzo: Utukufu Wa Masjid Al-Haraam Na Maharamisho Yake

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Utukufu Wa Masjid Al-Haraam Na Maharamisho Yake

 

 www.alhidaaya.com

 

 

وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُم مِّنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ ۚ وَالْفِتْنَةُ أَشَدُّ مِنَ الْقَتْلِ ۚ وَلَا تُقَاتِلُوهُمْ عِندَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ حَتَّىٰ يُقَاتِلُوكُمْ فِيهِ ۖ فَإِن قَاتَلُوكُمْ فَاقْتُلُوهُمْ ۗ كَذَٰلِكَ جَزَاءُ الْكَافِرِينَ ﴿١٩١﴾

191. Na wauweni popote muwakutapo, na watoeni popote walipokutoeni. Na fitnah ni mbaya zaidi kuliko kuua. Na wala msipigane nao kwenye Al-Masjidil-Haraam mpaka wakupigeni humo, watakapokupigeni basi wauweni. Namna hivi ndivyo jazaa ya makafiri.

 

 

Mafunzo

 

 

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika mji huu Ameuharamishwa Allaah tokea Siku Aliyoumba mbingu na ardhi. Hivyo, ni sehemu tukufu kwa amri ya Allaah mpaka Siku ya Qiyaamah. Kupigana kwake kulihalalishwa kwangu tena kwa saa chache mchana. Hivyo, ni sehemu tukufu kwa amri ya Allaah mpaka Siku ya Qiyaamah. Miti yake isikatwe na majani yasing’olewe. Endapo mtu atataja mapigano yaliyofanywa na Rasuli wa Allaah kuwa ni hoja inayoruhusu watu kupigana katika mji huo, basi semeni kuwa: Allaah Alimruhusu Rasuli Wake lakini hakukuruhusuni nyinyi.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Share