197-Aayah Na Mafunzo: Miezi Ya Hajj Na Haramisho La Maasi
Aayah Na Mafunzo
Al-Baqarah
Miezi Ya Hajj Na Haramisho La Maasi
الْحَجُّ أَشْهُرٌ مَّعْلُومَاتٌ ۚ فَمَن فَرَضَ فِيهِنَّ الْحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي الْحَجِّ ۗ وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ يَعْلَمْهُ اللَّـهُ ۗ وَتَزَوَّدُوا فَإِنَّ خَيْرَ الزَّادِ التَّقْوَىٰ ۚ وَاتَّقُونِ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ ﴿١٩٧﴾
197. Hajj ni miezi maalumu. Na atakayekusudia kuhiji (akahirimia), basi asifanye tendo la ndoa wala ufasiki wala mabishano katika Hajj. Na lolote mlifanyalo katika ya kheri Allaah Analijua. Na chukueni masurufu. Na hakika bora ya masurufu ni taqwa. Na nicheni Mimi enyi wenye akili!
Mafunzo:
Kuhusu miezi ya Hajj; Ibn ‘Umar (رضي الله عنه) alisema: Ni Shawwaal, Dhul-Qa’dah na siku kumi za mwanzo za Dhul-Hijjah. [Fat-hul-Baariy (3/491)]
Na kuhusu kubishana, imeharamsihwa khaswa katika Hajj na masiku yote yote mengineyo; Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mimi ni mdhamini wa nyumba ya kando ya Jannah kwa anayeacha mabishano hata kama ni mwenye haki, na ni mdhamini wa nyumba iliyo katikati ya Jannah kwa anayeacha uongo japo ni kwa mzaha, na mdhamini wa nyumba iliyo mahala pa juu zaidi ya Jannah kwa ambaye tabia yake ni njema.” [Abuu Daawuwd kwa isnaad Swahiyh]