224-Aayah Na Mafunzo: Makatazo Ya Kuendeleza Viapo Vya Makosa

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Makatazo Ya Kuendeleza Viapo

 

وَلَا تَجْعَلُوا اللَّـهَ عُرْضَةً لِّأَيْمَانِكُمْ أَن تَبَرُّوا وَتَتَّقُوا وَتُصْلِحُوا بَيْنَ النَّاسِ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٢٤﴾

224. Na wala msifanye (Jina la) Allaah kuwa ni nyudhuru ya viapo vyenu kukuzuieni katika kutenda wema na kuwa na taqwa na kusuluhisha baina ya watu. Na Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 Mafunzo :

Kutoka kwa Naafi’ kwamba Ibn ‘Umar alikuwa akisema katika Al-Iylaa (mwanamume kuapa kutokukutana na mkewe) Aliyoitaja Allaah (تعالى).

 

Makatazo ya kuendeleza viapo vya makosa: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Wa-Allaahi! Ni dhambi zaidi kwa Allaah, mmoja wenu anapotekeleza kiapo chake kuhusu (kuvunja uhusiano) na jamaa zake kuliko (kuvunja kiapo na) kulipa kafara (fidia) kama inavyotakiwa na Allaah katika hali kama hizi.” [Muslim]

 

 

 

Share