227-Aayah Na Mafunzo: Haramisho La Mwanamke Kuomba Talaka Bila Sababu
Aayah Na Mafunzo
Al-Baqarah
Haramisho La Mwanamke Kuomba Talaka Bila Sababu
وَإِنْ عَزَمُوا الطَّلَاقَ فَإِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿٢٢٧﴾
227. Na wakiazimia talaka, basi hakika Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.
Mafunzo:
Mwanamke haifai kuomba talaka bila ya sababu:
عَنْ ثَوْبَان مَوْلَى رَسُول اللَّه – صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ – عَنْ النَّبِيّ – صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ – أَنَّهُ قَالَ :((أَيّمَا اِمْرَأَة سَأَلَتْ زَوْجهَا الطَّلَاق فِي غَيْر مَا بَأْس حَرَّمَ اللَّه عَلَيْهَا رَائِحَة الْجَنَّة)) الترمذي و قال حديث حسن
Kutoka kwa Thawbaan amesema kwamba: Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mwanamke yeyote anayemuomba mumewe talaka bila ya sababu yoyote, Allaah Amemharimishia harufu ya Pepo” [At-Tirmidhiy na kasema Hadiyth Hasan]
Na riwaayah nyengine amesema:
“Mwanamke yeyote mwenye kumuomba mumewe talaka pasi na kosa lolote basi Jannah itakuwa haram kwake wala hatosikia harufu yake.” [Al-Bukhaariy, Muslim, Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy na Ibn Maajah].