282-Aayah Na Mafunzo: Aayah Ya Deni, Maana Ya Upungufu Wa Akili Kwa Wanawake
Aayah Na Mafunzo
Al-Baqarah
Aayah Ya Deni Maana Ya Upungufu Wa Akili Kwa Wanawake
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا تَدَايَنتُم بِدَيْنٍ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى فَاكْتُبُوهُ ۚ وَلْيَكْتُب بَّيْنَكُمْ كَاتِبٌ بِالْعَدْلِ ۚ وَلَا يَأْبَ كَاتِبٌ أَن يَكْتُبَ كَمَا عَلَّمَهُ اللَّـهُ ۚ فَلْيَكْتُبْ وَلْيُمْلِلِ الَّذِي عَلَيْهِ الْحَقُّ وَلْيَتَّقِ اللَّـهَ رَبَّهُ وَلَا يَبْخَسْ مِنْهُ شَيْئًا ۚ فَإِن كَانَ الَّذِي عَلَيْهِ الْحَقُّ سَفِيهًا أَوْ ضَعِيفًا أَوْ لَا يَسْتَطِيعُ أَن يُمِلَّ هُوَ فَلْيُمْلِلْ وَلِيُّهُ بِالْعَدْلِ ۚ وَاسْتَشْهِدُوا شَهِيدَيْنِ مِن رِّجَالِكُمْ ۖ فَإِن لَّمْ يَكُونَا رَجُلَيْنِ فَرَجُلٌ وَامْرَأَتَانِ مِمَّن تَرْضَوْنَ مِنَ الشُّهَدَاءِ أَن تَضِلَّ إِحْدَاهُمَا فَتُذَكِّرَ إِحْدَاهُمَا الْأُخْرَىٰ ۚ وَلَا يَأْبَ الشُّهَدَاءُ إِذَا مَا دُعُوا ۚ وَلَا تَسْأَمُوا أَن تَكْتُبُوهُ صَغِيرًا أَوْ كَبِيرًا إِلَىٰ أَجَلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ أَقْسَطُ عِندَ اللَّـهِ وَأَقْوَمُ لِلشَّهَادَةِ وَأَدْنَىٰ أَلَّا تَرْتَابُوا ۖ إِلَّا أَن تَكُونَ تِجَارَةً حَاضِرَةً تُدِيرُونَهَا بَيْنَكُمْ فَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَلَّا تَكْتُبُوهَا ۗ وَأَشْهِدُوا إِذَا تَبَايَعْتُمْ ۚ وَلَا يُضَارَّ كَاتِبٌ وَلَا شَهِيدٌ ۚ وَإِن تَفْعَلُوا فَإِنَّهُ فُسُوقٌ بِكُمْ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ وَيُعَلِّمُكُمُ اللَّـهُ ۗ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٢٨٢﴾
282. Enyi walioamini! Mtakapokopeshana deni mpaka muda maalumu uliopangwa, basi liandikeni. Na aandike baina yenu mwandishi kwa uadilifu. Na wala asikatae mwandishi kuandika kama Allaah Alivyomfunza. Basi aandikishe kwa imla yule ambaye ana haki (mdai) na amuogope Allaah, Rabb wake, na wala asipunguze humo kitu chochote. Basi ikiwa yule ambaye ana haki amepumbaa kiakili au mnyonge, au hawezi kuandikisha mwenyewe, basi aandikishe msimamizi wake kwa uadilifu. Na mshuhudishe mashahidi wawili wanaume miongoni mwenu. Na ikiwa hakuna wanaume wawili, basi mwanamme mmoja na wanawake wawili katika wale mnaowaridhia miongoni mwa mashahidi, ili kama mmoja wao hao wanawake wawili akikosea (akasahau), basi mmoja wao atamkumbusha mwengine. Na mashahidi wasikatae watapoitwa. Na wala msichukie kuliandika (deni) dogo au kubwa mpaka muda wake. Hivyo kwenu ndiyo uadilifu upasavyo mbele ya Allaah na ndio unyoofu zaidi kwa ushahidi; na ni karibu zaidi ili msiwe na shaka; isipokuwa itakapokuwa biashara taslimu mnayoiendesha baina yenu, basi si dhambi kwenu msipoiandika. Na shuhudisheni mnapouziana. Na wala asidhuriwe mwandishi wala shahidi; na mkifanya basi hakika huo ni ufasiki kwenu. Na mcheni Allaah, na Allaah Anakufunzeni, na Allaah kwa kila kitu ni Mjuzi
Mafunzo:
Hii ni Aayah ndefu kabisa kuliko zote katika Qur-aan na Aayah hii inajulikana kwa ‘Aayatud-dayn’ (Aayah ya deni).
Kuhusu upungufu wa akili na Dini kwa wanawake imekusudiwa katika maelezo yanayoendeleza Hadiyth “…Ama upungufu katika akili yake ni ushahidi wa wanawake wawili kwamba ni sawa na ushahidi wa mwanamme mmoja, na huo ndio udhaifu wa akili. Ama upungufu katika Dini, wanawake wakati mwengine (katika hedhi) hawaswali na kufunga Swiyaam mwezi wa Ramadhwaan.” [Muslim]