283-Aayah Na Mafunzo: Ruhusa Ya Kitu Rehani
Aayah Na Mafunzo
Al-Baqarah
Ruhusa Ya Kuweka Kitu Rehani
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
وَإِن كُنتُمْ عَلَىٰ سَفَرٍ وَلَمْ تَجِدُوا كَاتِبًا فَرِهَانٌ مَّقْبُوضَةٌ ۖ فَإِنْ أَمِنَ بَعْضُكُم بَعْضًا فَلْيُؤَدِّ الَّذِي اؤْتُمِنَ أَمَانَتَهُ وَلْيَتَّقِ اللَّـهَ رَبَّهُ ۗ وَلَا تَكْتُمُوا الشَّهَادَةَ ۚ وَمَن يَكْتُمْهَا فَإِنَّهُ آثِمٌ قَلْبُهُ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ ﴿٢٨٣﴾
283. Na mkiwa safarini na hamkumpata mwandishi, basi (mdai) akabidhiwe rahani. Na ikiwa mmoja wenu amewekewa amana na mwengine, basi airudishe yule ambaye ameaminiwa amana ya mwenzake; na amche Allaah, Rabb wake; na wala msifiche ushahidi; na mwenye kuuficha basi hakika moyo wake ni wenye kutenda dhambi. Na Allaah kwa mnayoyatenda ni Mjuzi.
Mafunzo:
‘Aaishah (رضي الله عنها) amehadithia kwamba “Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alinunua chakula kwa Yahudi lakini akamlipa muda ujao (deni). Na akaweka rehani nguo yake ya vita iliyotengenezwa kwa chuma.”
Sumurah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mkono wa mkopaji utabeba mzigo wa kile ulichochukua mpaka utakapolipa.” [Ahmad, Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy katika Al-Kubraa na Ibn Maajah]