285-Aayah Na Mafunzo: Fadhila Za Aayah Mbili Za Mwisho Suwratul-Baqarah
Aayah Na Mafunzo
Al-Baqarah
Fadhila Za Aayah Mbili Za Mwisho Suwratul-Baqarah
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa:
آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ ۚ كُلٌّ آمَنَ بِاللَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّن رُّسُلِهِ ۚ وَقَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۖ غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ ﴿٢٨٥﴾
285. Rasuli ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Rabb wake na Waumini (pia). Wote wamemwamini Allaah, na Malaika Wake, na Vitabu Vyake, na Rusuli Wake. (Nao husema): “Hatutofautishi baina ya yeyote kati ya Rusuli Wake.” Na wakasema: “Tumesikia na tumetii, tunakuomba maghfirah Rabb wetu na Kwako ni mahali pa kuishia.”
لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۚ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ ۗ رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلْنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِ ۖ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا ۚ أَنتَ مَوْلَانَا فَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ ﴿٢٨٦﴾
286. Allaah Hakalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake. Itapata (thawabu) iliyoyachuma, na ni dhidi yake (kwa maovu) iliyojichumia. “Rabb wetu Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Rabb wetu, Usitubebeshe mzigo kama Ulivyoubebesha juu ya wale waliokuwa kabla yetu. Rabb wetu, Usitutwike tusiyoyaweza, na Tusamehe, na Tughufurie na Turehemu, Wewe ni Mola Mlinzi wetu, basi Tunusuru dhidi ya watu makafiri.
Mafunzo:
Fadhila Za Aayah Mbili Za Mwisho Suwrah Al-Baqarah:
1-Kutokuhesabiwa katika kusahau na kukosea.
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:
إنَّ اللَّهَ تجاوزَ عن أمَّتيَ الخطأَ والنِّسيانَ ومَا استُكرِهُوا عليه
“Ummah wangu umenyanyuliwa makosa na kusahau na wanayo shurutishwa.” [Ibn Maajah, Ibn Hibbaan, Ad-Daraqutwniy, At-Twabaraniy na Al-Haakim, Irwaa Al-Ghaliyl (1027)]
2-Atakayezisoma zitamtosheleza:
عن أَبِي مَسْعُودٍ الأَنْصَارِيِّ، قَالَ قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم: ((الآيَتَانِ مِنْ آخِرِ سُورَةِ الْبَقَرَةِ مَنْ قَرَأَ بِهِمَا فِي لَيْلَةٍ كَفَتَاهُ))
Abuu Mas‘uwd Al-Answaariyy ‘Uqbah bin ‘Amr bin Tha’labah (رضي الله عنه) amesimulia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayesoma usiku Aayah mbili za mwisho wa Suwratul-Baqarah zitamtosheleza.” Yaani: zinamtosheleza kumkinga na kila baya na lenye kumdhuru. [Al-Bukhaariy na Muslim]
3-Hakuna Nabiy aliyepewa Aayah hizi isipokuwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)
عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ بَيْنَمَا جِبْرِيلُ قَاعِدٌ عِنْدَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم سَمِعَ نَقِيضًا مِنْ فَوْقِهِ فَرَفَعَ رَأْسَهُ فَقَالَ: ((هَذَا بَابٌ مِنَ السَّمَاءِ فُتِحَ الْيَوْمَ لَمْ يُفْتَحْ قَطُّ إِلاَّ الْيَوْمَ، فَنَزَلَ مِنْهُ مَلَكٌ فَقَالَ: هَذَا مَلَكٌ نَزَلَ إِلَى الأَرْضِ لَمْ يَنْزِلْ قَطُّ إِلاَّ الْيَوْمَ، فَسَلَّمَ وَقَالَ أَبْشِرْ بِنُورَيْنِ أُوتِيتَهُمَا لَمْ يُؤْتَهُمَا نَبِيٌّ قَبْلَكَ، فَاتِحَةُ الْكِتَابِ وَخَوَاتِيمُ سُورَةِ الْبَقَرَةِ لَنْ تَقْرَأَ بِحَرْفٍ مِنْهُمَا إِلاَّ أُعْطِيتَهُ)) .
Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesimulia: Jibriyl (عليه السّلام) alipokuwa na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alisikia sauti kutoka juu. Jibriyl (عليه السّلام) akatazama juu akasema: “Huu mlango wa mbinguni umefunguliwa na haujapatapo kamwe kufunguliwa isipokuwa leo.” Malaika akateremka humo akasema: “Huyu Malaika ameteremka ardhini, hajapatapo kuteremka kamwe isipokuwa leo.” Akasalimia kisha akasema: “Pokea bishara ya Nuru mbili ulizopewa ambazo hakuna Nabiy aliyepewa kabla yako; Ufunguo wa Kitabu (Al-Faatihah), na Aayah (mbili) za mwisho wa Suwratul-Baqarah. Hutosoma herufi humo ila utapewa barakah zake ziliomo.” [Muslim]
4-Aayah mbili hizi amepewa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa mbingu ya saba.
Hadiyth ya Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه):
لَمَّا أُسْرِيَ بِرَسُولِ اللّهِ صلى الله عليه وسلم انْتُهِيَ بِهِ إِلَى سِدْرَةِ الْمُنْتَهَى. وَهِيَ فِي السَّمَاءِ السَّادِسَةِ. إِلَيْهَا يَنْتَهِي مَا يُعْرَجُ بِهِ مِنَ الأَرْضِ. فَيُقْبَضُ مِنْهَا. وَإِلَيْهَا يُنْتَهِى مَا يُهْبَطُ بِهِ مِنْ فَوْقِهَا. فَيُقْبَضُ مِنْهَا. قَالَ: {إِذْ يَغْشَى السِّدْرَةَ مَا يَغْشَى} [النجم: 16] قَالَ: فَرَاشٌ مِنْ ذَهَبٍ. قَالَ: فَأُعْطِيَ رَسُولُ اللّهِ صلى الله عليه وسلم ثَلاَثاً: أُعْطِيَ الصَّلَوَاتِ الْخَمْسَ. وَأُعْطِيَ خَوَاتِيمَ سُورَةِ الْبَقَرَةِ. وَغُفِرَ لِمَنْ لَمْ يُشْرِكْ بِالله مِنْ أُمَّتِهِ شَيْئاً الْمُقْحِمَاتُ (رواه مسلم) .
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipopelekwa safari ya usiku mbinguni (Al-Israa Wal-Mi’raaj), aliishia Sidratul-Muntahaa (Mkunazi wa mpaka wa mwisho kabisa) katika mbingu ya sita ambapo huishia kila kitu (hakuna ajuaye ‘ilmu ya baada ya hapo isipokuwa Allaah). Ambapo pia kunaishia kila kinachopanda kutoka ardhini (amali za watu n.k) na kushikiliwa humo, na kinapoishia kila kitu kinachoteremka kutoka juu yake na kushikiliwa hapo. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
إِذْ يَغْشَى السِّدْرَةَ مَا يَغْشَىٰ ﴿١٦﴾
Ulipoufunika mkunazi huo unachokifunika [An-Najm: 16]
(Msimulizi) Akasema: Vipepeo vya dhahabu. Akasema: Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akapewa (mambo) matatu: Akapewa Swalaah tano za kila siku. Na akapewa hitimisho la Suwrah Al-Baqarah. Na kughufuriwa katika Ummah wake ambaye hamshirikishi Allaah na chochote. [Muslim]